MARADONA BADO ANAENDELEZA MALUMBANO NA NCHI YAKE
NGULI wa zamani wa Soka
wa Argentina, Diego Maradona ameendelea na ugomvi wake wa kipindi kirefu
na nchi hiyo baada ya kutangaza kuwa hataiunga mkono timu ya taifa ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Argentina ambayo itashiriki michuano
ya Kombe la Dunia huko Falme za Kiarabu-UAE.
Nyota
huyo wa zamani wa klabu ya Napoli ya Italia, bado hajamaliza tofauti
zake na Chama cha Soka cha Argentina-AFA toka alipotimuliwa nafasi ya
ukocha katika timu ya wakubwa ya nchi hiyo baada ya michuano ya Kombe la
Dunia 2010. Maradona
kwasasa ni mshauri wa klabu ya Deportivo Riestra ya nchini kwake na pia
ni balozi wa michezo wa Dubai baada ya kuacha kuifundisha klabu ya Al
Wasl mwaka jana. Akizungumza
na waandishi wa habari, Maradona amesema ataiunga mkono timu ya taifa
ya UAE katika michuano hiyo na sio Argentina kwasababu ya matatizo yake
na AFA.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!