KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Emmanuel Frimpong, ambaye
anaichezea Arsenal, soka lake la klabu limeingia walakini baada ya timu
hiyo vinara wa Ligi Kuu England, kusema inatafuta timu ya kumnunua ili
imwondoe klabuni hapo.

Kutokana na kuwapo kwa mpango huo, huenda Frimpong
akafunguliwa mipango ya kuondoka Emirates katika kipindi cha usajili wa
dirisha dogo kitakachofanyika Januari mwakani.

Arsenal inataka kumpeleka Frimpong kwenye klabu za Championship baada ya pia kumweleza mwenyewe kwamba anaruhusiwa kuondoka.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!