Home »
siasa afrika
» OBAMA ATOWA ONYO KALI ZIDI YA VIKOSI VYA WAASI SUDAN KUSINI
OBAMA ATOWA ONYO KALI ZIDI YA VIKOSI VYA WAASI SUDAN KUSINI
Rais wa Marekani Barack Obama jana
Jumamosi amevionya vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini dhidi ya
mapinduzi ya kijeshi baada ya wanajeshi wanne wa Marekani kujeruhiwa
katika shambulizi dhidi ya ndege yao wakati wakijielekeza mjini Bor kwa
shughuli za uokozi.
Taarifa ya ikulu ya Marekani imeeleza kuwa juhudi zozote za kunyakua
madaraka kwa nguvu za kijeshi zitasababisha kukoma kwa msaada wa muda
mrefu kutoka Marekani jumuiya ya kimataifa.
Rais Obama amesisitiza kuwa viongozi wa Sudani Kusini wanalo jukumu
la kusaidia juhudi za Marekani kuwaokoa wamarekani na raia huko Juba
na Bor mji ambao unashikiliwa na waasi.
Onyo la rais Obama linakuja baada ya ndege tatu za Marekani
kushambuliwa kwa risasi wakati zikielekea huko Bor kusaidia juhudi za
kuwaondoa wa Marekani nchini Sudani Kusini kufuatia kuchacha kwa
mapigano baina ya serikali na waasi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!