Home »
siasa kimataifa
» RAIA WANAOPINGA UTAWALA WA SASA WA THAILAND WAANDAMANA WAKIMTAKA WAZIRI MKUU AJIUZULU
RAIA WANAOPINGA UTAWALA WA SASA WA THAILAND WAANDAMANA WAKIMTAKA WAZIRI MKUU AJIUZULU
Watu wanaoipinga serikali ya Thailand wamefanya maandamano mengine
makubwa wakiendelea kuishinikiza serikali ya uangalizi na kutaka waziri
mkuu Bibi Yingluck Shinawatra ajiuzulu na kuahirisha uchaguzi mkuu
uliopangwa kufanyika Februari mwaka kesho. Kabla ya maandamano hayo,
kiongozi wa maandamano Bw Suthep Taugsuban alieleza kitakachofanyika.
"Naamini watu zaidi ya milioni 3 watashiriki kwenye maandamano ya
leo. Kama Yingluck hatajiuzulu, tutaendelea na maandamano, leo
tunasimamisha mawasiliano ya barabarani kwa nusu siku, na safari
nyingine tutasimamisha kwa siku nzima."
Lakini takwimu za polisi zimesema, idadi ya waandamanaji ilifikia laki 1.5.
Maandamano ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa nchini
Thailand katika miezi miwili iliyopita. Hapo awali waziri mkuu Bibi
Yingluck alivunja bunge kujibu matakwa ya waandamanaji, na kutangaza
siku ya uchaguzi, lakini waandamanaji hawakuridhika na matokeo hayo na
kutaka Bibi Yingluck mwenyewe kujiuzulu na kuahirisha uchaguzi
uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwakani ili kupata muda wa mwaka
mmoja na nusu wa kujindaa kwa uchaguzi mkuu na kufanya mageuzi.
Hata hivyo, tume ya uchaguzi wa nchi hiyo imesisitiza kuwa
uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kuanza leo hautaahirishwa. Lakini wakati huohuo watu wa hali mbalimbali
ya jamii ya Thailand wameeleza matakwa yao ya kutaka mageuzi yafanyike.
Chama kikubwa zaidi cha upinzani cha Demokrasia kimeamua kususia
uchaguzi mkuu ujayo, kama anavyoeleza kiongozi wa chama hicho Bw Abhisit
Vejjajiwa.
"Tumeamua kutoshiriki kwenye uchaguzi wa mwakani. Ningependa
kuwaambia wananchi wanaotaka kukipigia kura chama cha Demokrasia, kwamba
mageuzi ambayo mngependa kuyaona yatatimizwa, na siku hiyo itakapofika,
tutafanya mageuzi ya muda mrefu na kurudisha imani ya wananchi juu ya
demokrasia na mfumo wa bunge. Haya ndiyo matumaini ya chama cha
Demokrasia. Tumefanya uamuzi huu na tutaendelea nao."
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!