Home »
siasa afrika
» HOFU YAANZA KUTANDA KUSINI MWA NCHI YA DRC,YARIPOTIWA KUWEPO MAKUNDI YA WAASI
HOFU YAANZA KUTANDA KUSINI MWA NCHI YA DRC,YARIPOTIWA KUWEPO MAKUNDI YA WAASI
Mashirika ya utoaji misaada katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo yametangaza kuwa, maeneo ya kusini mwa nchi hiyo yameendelea
kushuhudia mashambulio ya makundi ya wanamgambo. Taarifa ya mashirika
hayo imebainisha kwamba, katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, watu
wasiopungua 60 wameuawa katika mji wa Katanga wa kusini mwa nchi hiyo
kufuatia mashambulio ya wanamgambo wanaojulikana kwa jina la Bakata
Katanga.
Ripoti ya mashirika ya misaada ya kibinaadamu imeeleza kuwa,
mashambulio ya wanamgambo hao katika maeneo hayo yamepelekea kwa akali
watu laki tano kuyakimbia makazi yao.
Afisa mmoja wa mashirika hayo ya misaada ya kibinadamu anayefanya
shughuli zake mjini Lubumbashi, makao makuu ya Katanga amewaambia
waandishi wa habari kwamba, shule, makanisa na vituo vya matibabu navyo
havijasalimika na mashambulio hayo ya waasi. Wanamgambo wa Katanga
wanaendesha mapambano dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo wakipigania kujitenga eneo la Katanga.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!