ITAKUWA balaa tena. Itatisha kwa mara nyingine. Ndivyo
Manchester United inavyotabiriwa kufufuka baada ya jana Ijumaa
kukamilisha uhamisho wa kiungo mchezeshaji wa Chelsea, Juan Mata.
Lakini hapo hapo imetabiriwa kuwa Mata si
suluhisho la matatizo yote ya Manchester United katika msimu huu ambao
wameonekana kuwa ovyo kupita kiasi.

“Baada ya msimu wa ovyo, mashabiki wa Manchester
United wamekuwa wakimtafuta shujaa. Kwa Juan Mata nadhani watakuwa
wamempata shujaa. Baada ya kichapo cha Sunderland, Mata ni alama ya
matumaini Old Trafford.” Alisema Redknapp.

“Manchester United inabidi iondokane na wachezaji
wengi ili warudi juu na wanahitaji wachezaji wenye ubora kama sita
hivi.Wachezaji kama Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand
wataondoka katika kipindi cha majira ya joto, ni wakati wa kuanzisha
mradi mwingine. Lakini hata hivyo usajili wa Mata ni mwanzo mzuri.”
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alithibitisha kiungo huyo kutimkia Manchester United baada ya kupokea ofa nzuri.

Mata alitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na
atalipwa Pauni 140,000 kwa wiki huku akiwa mchezaji ghali zaidi katika
rekodi ya Manchester United akisajiliwa kwa Pauni 37 milioni.
Ana kazi kubwa ya kurudisha matumaini ya mashabiki
wa Manchester United ambayo mpaka sasa inashika nafasi ya saba katika
msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa wameachwa kwa pointi 14 na vinara
Arsenal.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!