Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , , » BADO ULE MGANGA ALIYE JITANGAZA KUMROGA CHRISTIANO RONALDO ANAENDELEA KUMTENGENEZAA TENGENEZAA

BADO ULE MGANGA ALIYE JITANGAZA KUMROGA CHRISTIANO RONALDO ANAENDELEA KUMTENGENEZAA TENGENEZAA

Written By Unknown on Friday 6 June 2014 | Friday, June 06, 2014

Maneno ya mganga wa kienyeji wa Ghana, Nana Kwaku Bonsam, yameanza kudhihirika baada ya uongozi wa timu ya taifa ya Ureno kuthibitisha taarifa za mshambuliaji Cristiano Ronaldo, kutokuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno ambacho hii leo kinacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mexico.
Nana Kwaku Bonsam, amesema yeye ndiye anayemroga nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno, ili asicheze mchezo wa kundi la saba katika fainali za kombe la dunia ambapo timu ya taifa ya Ureno itapambana na timu ya taifa ya Ghana, Black Stars.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paul Bento amesema pamoja na kutarajia kumkosa Ronaldo katika mchezo wa hii leo wa kirafiki, bado hajafahamu ni lini mshambuliaji huyo atakuwa fit kwa ajili ya kujiunga na wenzake.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Real Madrid anasumbuliwa na maumivu ya mishipa fulani laini katika mguu wake, ambapo kwa mara ya mwisho alionekana uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya walipocheza dhidi ya Atletico Madrid.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi