Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HABARI KUTOKA SUDAN ZASEMA KUWA KIONGOZI MWINGINGE WA UPINZANI AMETUPWA GEREZANI

HABARI KUTOKA SUDAN ZASEMA KUWA KIONGOZI MWINGINGE WA UPINZANI AMETUPWA GEREZANI

Written By Unknown on Monday 9 June 2014 | Monday, June 09, 2014

Polisi ya Sudan imemtia mbaroni kiongozi mwingine wa upinzani nchini humo. Ibrahim al-Sheikh mkuu wa chama cha Kongresi ya Sudan, ametiwa mbaroni mapema leo huko katika jimbo la Kordofan Magharibi, nchini humo. Ibrahim amekamatwa na polisi ya Sudan kwa tuhuma za kutoheshimu katiba, kueneza propaganda za uongo na kutishia usalama wa taifa. Katibu wa chama hicho, Abdelqayum Awad amesema kuwa, ikiwa tuhuma anazotuhumiwa Ibrahim zitathibiti dhidi yake, basi kuna uwezekano wa kuhukumiwa adhabu ya kifo. Itakumbukwa kuwa wiki tatu zilizopita, maafisa wa usalama wa nchi hiyo, walimtia mbaroni Sadiq al-Mahdi, mkuu wa chama cha Umma aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Sudan kwa tuhuma za uchochezi dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir, suala lililopelekea wafuasi wa kiongozi huyo kuandamana siku ya Ijumaa wakiishinikiza serikali ya Khartoum kumuachilia huru kiongozi wao huyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi