Home »
siasa afrika
» HALI YA MACHAFUKO INAYO ZIDI KUENDELEA KURIPOTIWA SUDAN KUSINI YAITIYA HOFU UMOJA WA MATAIFA(U.N)
HALI YA MACHAFUKO INAYO ZIDI KUENDELEA KURIPOTIWA SUDAN KUSINI YAITIYA HOFU UMOJA WA MATAIFA(U.N)
Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani kuendelea
umwagaji damu nchini Sudan Kusini kutokana na kutoheshimiwa makubaliano
ya usitishaji vita na kuzitaka pande hasimu za mgogoro wa nchi hiyo
kuacha operesheni zote za kijeshi na kushikamana na ahadi za huko nyuma.
Ban amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na Rais Salva Kiir wa
nchi hiyo.
Aidha katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake
kutokana na kuendelea uadui ambao ni kinyume na makubaliano ya Januari
23 ya kuacha uadui, na pia makubaliano ya Mei 9 yaliyotiwa saini kati
ya Rais Salva Kiir na makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek
Machar.
Mapigano nchini Sudan Kusini yamepelekea maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni 1.3 kuwa wakimbizi.
Umoja wa Mataifa huko nyuma ulisema pia kuwa, kuheshimiwa usitishaji
mapigano ni muhimu ili kuboresha hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa
katika nchi hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!