Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULIFAHAMU SABABU ZA TUNISIA NA MISRI KUFUNGA MIPAKA YAO YOTE INAYO INGIA LIBYA? HIZI HAPA UNAWEZA KUZISOMA.

JE,ULIFAHAMU SABABU ZA TUNISIA NA MISRI KUFUNGA MIPAKA YAO YOTE INAYO INGIA LIBYA? HIZI HAPA UNAWEZA KUZISOMA.

Written By Unknown on Friday 22 August 2014 | Friday, August 22, 2014

Nchi za Misri na Tunisia zimefunga mipaka yao ya anga na nchi jirani ya Libya.
Shirika la Ndege la Tunisia na mamlaka ya uwanja wa ndege wa Cairo nchini Misri zimetangaza kuwa zimefuta safari zote za kuelekea au kutoka Libya kutokana na machafuko na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.
Ripoti zinasema kuwa mapigano makali yaliyoanza Jumatano iliyopita yanaendelea katika mji wa Benghazi ulioko kaskazini mashariki mwa Libya. Vilevile mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli umetumbukia katika mapigano makali kati ya makundi ya wanamgambo hasimu yanayoendelea kwa wiki kadhaa sasa.
Serikali ya Libya imetangaza kuwa ndege za kivita za upande usiojulikana zinashiriki katika mapigano hayo tangu Jumatatu iliyopita.
Siku chache zilizopita Bunge jipya la Libya limeuomba rasmi Umoja wa Mataifa uisaidie nchi hiyo kukabiliana na machafuko. Bunge la Libya liliutaka Umoja wa Mataifa utume majeshi ya kuwalinda raia na kurejesha utulivu nchini humo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi