MCHEZAJI mpya ghali wa Arsenal, Mesut
Ozil, ambaye amebeba mustakabali wa kocha Arsene Wenger kubaki au
kuondolewa akichemsha mwishoni mwa msimu, ameanza kazi vyema akiiwezesha
Gunners kushinda 3-1 ugenini dhidi ya Sunderland.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani
aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42 kutoka Real Madrid siku ya mwisho ya
usajili, aling'ara mno Jumamosi wakati Arsenal ikipata ushindi huo
mnono.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Atkinson, mabao ya Arsenal yalifungwa na Giroud
dakika ya 11 na Aaron Ramsey mawili, dakika za 67 na 76, wakati bao
pekee la Sunderland lilifungwa na Gardner dakika ya 48.
Kikosi cha Sunderland kilikuwa: Westwood,
Celustka, Diakite, Roberge, Colback; Vaughan/Gardner dk46, Ki 6,
Johnson, Fletcher/Wickham dk77, Altidore na Mavrias/Borini dk72.
Arsenal: Szczesny,
Jenkinson, Sagna, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere, Ozil/Vermaelen
dk80, Ramsey, Walcott/Monreal dk88 na Giroud/Akpon dk90+3.
|
Mtu muhimu: Aaron Ramsey akifunga bao la tatu |
|
Mtu mkubwa: Mesut Ozil ameng'ara akiichezea Arsenal kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 42 |
|
Ozil anatoa pande |
|
La kwanza: Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud (kulia) akifunga bao la kwanza Uwanja wa Light |
|
Mesut Ozil (kulia) akimpongeza Giroud |
Naye kocha Manuel Pellegrini ameshindwa kufurukuta mbele ya Stoke City baada ya kulazimishwa sare 0-0.
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross,
Huth, Pieters, Walters, Nzonzi, Wilson, Adam/Arnautovic dk70,
Etherington/Ireland dk70 na Jones/Crouch dk77.
Man City: Hart, Zabaleta, Garcia, Nastasic, Kolarov, Toure, Rodwell, Milner, Jovetic/Aguero dk63, Nasri/Navas dk73 na Negredo.
|
Mshambuliaji wa Manchester City, Stevan Jovetic (kushoto) akisikitika baada ya kukosa bao |
Nayo Manchester United imeibuka na
ushindi wa 2-0 dhidi ya Cyrstal Palace na kumpa faraja wake kocha wake
mpya, David Moyes katika mechi ambayo kocha wa zamani wa Mashetani hao
Wekundu alikuwepo uwanjani kushuhudia.
Mabao ya United yalifungwa na Robin van Persie kwa penalti dakika ya 45 na Wayne Rooney dakika ya 81.
Kikosi cha Man United kilikuwa: De Gea, Fabio, Ferdinand, Vidic, Evra , Anderson/Fellaini dk61, Carrick, Valencia, Rooney, Young/Januzaj dk66 na Van Persie.
Crystal Palace: Speroni, Mariappa,
Gabbidon, Delaney, Moxey, Dikgacoi, Jedinak, Puncheon, Gayle/Jerome
dk63, Campana/Guedioura dk58, Chamakh/Kebe dk74.
|
akienda chini ndani ya eneo la hatari kuipatia United penalti |
|
Nyekundu: Kagisho Dikgacoi alipewa kadi nyekundu na refa Jon Moss |
|
Kitu na boksi: Robin van Persie akiifungia United kwa penalti |
|
Wayne Rooney akipiga mpira wa adhabu kufunga |
|
Furaha imerejea: Rooney akishangilia bao lake |
|
Young akienda chini tena |
|
Wayne Rooney akiwapungia mashabiki |
|
Not affected: Rooney went about his business and scored a free-kick, with a headband covering his cut |
|
Go on son: David Moyes threw on new recruit Marouane Fellaini as a second-half substitute |
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!