BABA wa kiungo wa
kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil ametishia kuchukua hatua za kisheria
baada ya madai ya vyombo vya habari nchini Hispania kwamba mchezaji huyo
alikuwa amebanwa na mambo binafsi wakati akiwa Real Madrid. Mapema
wiki hii gazeti la ABC lilimkariri rais wa Madrid, Florentino Perez
akidai anaamini Ozil hakuwa mchezaji mwenye weledi kwasababu maisha yake
akiwa huko yalitawaliwa na wanawake na starehe za usiku. Lakini
Mustafa ambaye ndio baba yake Ozil amejibu tuhuma hizo na kudai ni za
kipuuzi kwani mwanae alikuwa akijitoa wakati akiwa Madrid ndio maana
alikuwa akicheza mara nyingi. Mustafa
amesema wanataka kumlaumu mwanae hivi sasa kwasababu mashabiki na
wachezaji wenzake wamekasirishwa na uamuzi wa klabu hiyo kumuuza. Ozil
ambaye amefunga na kusaidia mabao 108 katika mechi 159 alizocheza akiwa
Madrid alikamilisha umamisho wake kwenda Arsenal katika dakika za
mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa wenye thamani ya euro
milioni 50 na kuwashangaza wachezaji wenzake wengi.
Home »
michezo ulaya
» BABA YAKE OZIL ATISHIA KUWAPELEKA POLISI WANAMSHUTUMU MWANAE KUPENDA KULA BATA.
BABA YAKE OZIL ATISHIA KUWAPELEKA POLISI WANAMSHUTUMU MWANAE KUPENDA KULA BATA.
Written By Unknown on Thursday, 12 September 2013 | Thursday, September 12, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!