MSHAMBULIAJI Mario Balotelli ameinusuru
AC Milan kulala baada ya kufunga kwa penalti na kufanya sare ya 2-2 na
Torino, ambao walikuwa wanapigania ushindi wa kwanza The Rossoneri ndani
ya miaka 12.
Macho ya wengi yalikuwa kwa Kaka, ambaye
alikuwa anarejea rasmi Milan baada ya miaka minne ya kuitumikia Real
Madrid, lakini Torino ikatangulia kupata mabao mawili kipindi cha pili.
Nahodha, Danilo D'Ambrosio na Alessio
Cerci waliifungia mabao hayo Il Toro na kuiatamanisha ushindi wa kwanza
dhidi ya Milan tangu Novemba 2001 na Sulley Muntari akaipunguzia
Rossoneri bao moja baadaye, kabla ya Balotelli kusawazisha kwa penalti
dakika ya 90.
Wakati huo huo, Napoli ilishinda 2-0 dhidi ya Atalanta Uwanja wa Stadio San Paolo na kupanda kileleni.
Timu ya Rafael Benitez.
|
Mkali wa matuta: Mario Balotelli akipiga penalti iliyoinusuru Milan |
|
Balotelli baada ya kufunga |
|
Amerudi: Kaka alipewa beji ya Unahodha wa AC Milan jana baada ya kurejea kutoka Real Madrid |
|
Kaka jana akiichezea kwa mara ya kwanza AC Milan baada ya kurejea |
|
. |
|
Kileleni: Kocha wa Napoli, Rafa Benitez ameifunga Atalanta na kuendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 Serie A msimu huu |
|
. |
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!