BAADA ya kupata kashfa za tuhuma za kuiba beat na wazo la nyimbo za
wasanii wenzake, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul
Diamond Platinum' ameweka msimamo wa kutofanya kazi yoyote na wasanii wa
hapa nyumbani.
Msimamo wa msanii huyo umetokana na tuhuma alizopata zilizodai kuiba beat ya msanii mwenzake Dayna pamoja na kitikio cha wimbo cha Baba levo, ambapo tuhuma hizo ziliibuka baada ya Diamond kuachia wimbo wake unaojulikana kwa jina la 'Number One'.
Akifanya mahojiano katika kipindi cha XXL kinachorushwa na redio Clouds, msanii huyo aliweka wazi kuwa tuhuma anazozipata zinamuhuzunisha hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi na msanii yeyeto yule.
"Mimi sasa naamua kutofanya kazi na msanii yeyote yule kwani kila siku watu wanatafuta visa ili wapate majina matokeo yake wanatafuta visa vya kunichafua wakati mimi naweka hela nyingi katika muziki wangu" alilalamika Diamond.
Akizungumzia kashfa anazozipata juu ya kutuhumiwa kuiba nyimbo za baadhi ya wasanii wenzake aliweka wazi kuwa kutokana na kitendo hicho hatoweza kukubari kufanya kazi na msanii yeyeto yule, hivyo atabaki kufanya kazi zake peke yake ili asiharibu soko la muziki wake.
Msanii huyo ni mara ya pili sasa anaingia katika tuhuma za kutuhumiwa kuiba mawazo ya nyimbo za wasanii wenzake ambapo mara ya kwanza ilisemekana nyimbo ya 'Nataka kulewa' amemwiibia H. Baba.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!