Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Ethiopia yasisitiza kupatika amani Somalia

Ethiopia yasisitiza kupatika amani Somalia

Written By Unknown on Monday, 16 September 2013 | Monday, September 16, 2013


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amesisitiza juu ya kurejesha amani huko Somalia. Tedros Adhanom Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amesema Addis Ababa inasisitiza kuendelezwa jitihada zilizokwishaanzishwa kwa ajili ya kurejesha amani na utulivu nchini Somalia. Adhanom amesisitiza kuwa kuna ulazima wa kurejeshwa amani na utulivu na kuzingaiwa maslahi ya wananchi wa Somalia. Amesema Ethiopia inaunga mkono kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo na Somalia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia. Katika mazungumzo hayo Rais wa Somalia amesema pia kuwa Ethiopia imekuwa na nafasi muhimu katika kusogeza mbele mwenendo wa kusaka amani huko Somalia. Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia amepongeza pia juhudi za Addis Ababa katika kuboresha uhusiano wa nchi za Pembe ya Afrika na kustawisha sekta za biashara na uchumi katika eneo hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi