Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HIZI NDIO SABABU 4 ZINAZOFANYA MIDUME KUMTOLEA MACHO JOKETI NA KUMTAKA KIMAPENZI:

HIZI NDIO SABABU 4 ZINAZOFANYA MIDUME KUMTOLEA MACHO JOKETI NA KUMTAKA KIMAPENZI:

Written By Unknown on Friday, 13 September 2013 | Friday, September 13, 2013

 MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. 

Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
 

“Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.

“Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
 
Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.

Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi