Home »
michezo africa
» RATIBA YA TIMU 10 ZILIZOTINGA HATUA YA MTOANO KWA AFRIKA HADHARANI.
RATIBA YA TIMU 10 ZILIZOTINGA HATUA YA MTOANO KWA AFRIKA HADHARANI.
NCHI 10 za Afrika ambazo
zimetinga hatua ya mtoano ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani
zimejua hatma yao katika ratiba iliyopangwa katika makao makuu ya
Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF yaliyopo jiji Cairo, Misri. Timu
hizo ambazo ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, Misri,
Ethiopia, Ghana, Nigeria, Senegal na Tunisia ndio zinatafuta nafasi tano
za kwenda kushiriki michuano hiyo nchini Brazil. Katika
ratiba hiyo Ivory Coast ambao wataanzia nyumbani watakwaana na Senegal,
Ethiopia wataikaribisha Nigeria, Tunisia ambao waliingia katika hatua
hiyo kwa mlango wa pili wataanza na Cameroon nyumbani. Wengine ni Ghana watakaokwaana na Misri wakati Burkina Faso wenyewe wamepangwa kuchuana na Algeria. Mechi
hizo za mtoano zitachezwa kwa mikondo miwili ya nyumbani na ugenini
ambapo mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa kati ya Octoba 11 na 15 na
zile za mkondo wa pili zitachezwa kati ya Novemba 15 na 19 mwaka huu.
Côte d'Ivoire - Sénégal
Ethiopie - Nigeria
Tunisie - Cameroun
Ghana - Egypte
Burkina Faso - Algérie
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!