Lile bifu linalondelea kati ya mwigizaji Irene Uwoya na mmiliki wa kampuni maarufu ya magazeti nchini TANZANIA Erick Shigongo limeshika hatamu mpya baada ya mwigizaji huyo kuendelea kusema yake ya moyoni kuhusu kile ambacho anakisema kuendelea kuchafuliwa na mfanyibiashara huyo kupitia magazeti yake hayo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Irene ameandika...
“…Ipo siku ntaongea ukweli kuhusu shigongo na ushaid pia
ntatoa...usilo lijua nikama usiku wagiza ndomana atawadanganya wasio na
akili na wasio mjua....ntapgana nae mpaka tone la mwisho la damu yangu
ntasema kila kitu kwanin ananichukia...na ntaweka kila kitu waz....then
wenye akili watajua naongea nin...simuogop atakama atanichafua kiasi
gan...hizo kwangu ni matone yamvua bado mvua yenyewe...I don care
kwaatakae muamin but mwisho wa siku ukweli utaonekana na atataman ardhi
ipasuke......mim irene uwoya sijashawishiwa na mtu wala kulazimishwa
naahidi ya kwamba ntaongea…”Hayo ni maneno ya mwanadada huyu kuhusu linachoendelea kati ya na Erick Shigongo.
Baadaye tutafanya mawasiliano na Irene Uwoya ili tuweze kuwaletea undani halisi wa sakata hilililianza Jumamosi ya wiki iliyopita baada ya gazeti la Risasi ambalo linamilikiwa na
Globalpublishers lilikuwa na habari ya actress Irene Uwoya kudaiwa kuiba
simu. Uwoya anadai kuchafuliwa na Shigongo na ipo siku ataweka kila
kitu wazi ili watu waujue ukweli. Kupitia Instagram Irene ambaye mwaka
huu ameonekana kwenye filamu nyingi na kuanzisha kipindi cha Tv cha Paradise haya ndio aliyo andika......



0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!