Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Kirusi hatari chaua watu 2 Saudi Arabia

Kirusi hatari chaua watu 2 Saudi Arabia

Written By Unknown on Monday, 16 September 2013 | Monday, September 16, 2013



Kirusi cha Kirusi cha MERS-CoV kinavyoonekana katika mikroskopu
Wanawake wawili wameaga dunia nchini Saudi Arabia baada ya kuambukizwa kirusi hatari kijulikanacho kwa jina la Middle East Respiratory Syndrome Coronavirus (MERS-CoV).
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya Saudi Arabia imeongeza kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 41 aliyekuwa akifanya kazi hospitalini ameaga dunia katika mji mkuu Riyadh, huku mwingine mwenye umri wa miaka 79 akipoteza maisha katika eneo la Hafr al-Baten katika mkoa wa Mashariki.
Vifo vya wanawake hao wawili vimeongeza idadi ya watu walipoteza maisha kutokana na kirusi hicho nchini Saudi Arabia hadi 44. Mapema jana, Baraza Kuu la Afya nchini Qatar nalo lilitangaza kuwa mtu mmoja aliaga dunia Ijumaa nchini humo baada ya kuonyesha dalili za kirusi hicho cha MERS-Cov. Mwezi uliopita Wizara ya Afya ya Saudi Arabia ilitoa onyo kwa Mahujaji na kuwataka wavae barakoa katika maeneo yenye misongamano mikubwa ili kuzuia kuenea kirusi hicho hatari. Taarifa hivyo iliwataka wazee na wale wenye magonjwa sugu kuakhirisha safari za Hija au Umra mwaka huu.
Kirusi cha MERS-CoV kimesharipotiwa pia huko Imarati, Tunisia, Jordan, Uingereza, Ujerumani na Italia na kinashabihiana na kile cha SARS ambacho kiliua karibu watu 800 mwaka 2003.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi