Mfalme Mswati III wa Swaziland alipokuwa katika harusi ya Mwanamfalme William wa Uingereza na Kate Middleton, Aprili 29, 2011. |
MFALME wa Swaziland Mswati III amemteua
mwanamke wa umri wa miaka 18 anayeshindania tuzo ya urembo na anapangiwa
kumuoa awe mke wa 14.
Hayo yalitangazwa na msemaji wa ikulu Jumanne.
"Ninaweza kuthibitisha kwamba mfalme
ameletea taifa liphovela mpya (liphovela nni mchumba wa kifalme),”
gavana wa ikulu ya Ludzidzini Timothy Mtetwa alisema.
Mswati, mwenye umri wa miaka 45 ndiye mfalme wa pekee aliyesalia mwenye mamlaka makuu Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
Kwa mujibu wa Mtetwa, Mfalme Mswati III alimtambulisha mwanamke huyo kwa jina Sindiswa Dlamini wakati wa Densi ya Tete.
Alikuwa amevalia manyoya mekundi kichwani – ishara ya ufalme.
Mwanamke huyo alimaliza shule ya
upili ya St. Francis High School mjini Mbabane mwaka uliopita na akafika
fainali ya shindano la urembo la Miss Cultural Heritage. Mshindi
atatangazwa Septemba 28.
Harusi itafanyika tu ikiwa mchumba huyo atashika mimba. Dlamini wakati huo atakuwa mke wa 14 wa Mswati.
Wake watatu wametoroka nyumba ya
mfalme huyo miaka ya hivi majuzi. Wa majuzi zaidi, Malkia LaGija,
alitoroka ikulu 2012 akidai kwamba alikuwa akichapwa na kuteswa kiakili.
Kufumaniwa
Mwingine, LaDube, anadaiwa kupigwa
baada ya kupatikana akishiriki ngono na waziri wa haki, ambaye ni rafiki
wa karibu wa mfalme huyo.
Mswati alimteka nyara na kumuoa mfalme huyo akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2005.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!