Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MPYA! Mtoto wa Kike Ahitimu

MPYA! Mtoto wa Kike Ahitimu

Written By Unknown on Thursday, 12 September 2013 | Thursday, September 12, 2013

Kutojua kusoma na kuandika ni jambo ambalo linaweza kukuaibisha na linayaathiri maendeleo ya mtu binafsi.Hilo ndilo wanalolitambua ndugu wawili Latifa na Elinam katika makala haya mapya ya Noa Bongo-Jenga Maisha Yako.
Msichana akiwa shuleni
Kujua kusoma na  kuandika   pamoja na  elimu ni mambo muhimu yanayokubalika kuwa chachu  ya  maendeleo. Hatahivyo kiasi cha zaidi ya watu wazima milioni 150 kote  ulimwenguni  hawawezi kusoma na kuandika. Mwaka 2003 Shirika la Umoja wa Mataifa lilizindua rasmi muongo  wa kuzipa  msukumo harakati  za  kuiongeza idadi ya watu  wanaoweza kusoma na kuandika  ifikapo mwaka 2012. Elimu ,pia ni moja ya malengo ya milenia  ya maendeleo ya Umoja  wa  Mataifa.
Watoto wa kike wana uwezekano  mkubwa   zaidi wa kutopata elimu na wengi  wao hulazimika  kuacha  shule mapema pale  wazazi wanaposhindwa kuwalipia karo  wana  wao  wote ili waende shule kila  wakati.
Katika mchezo huu, Latifa  anakabiliwa  na  tatizo hilo ijapokuwa amekuwa akipata alama  nzuri shuleni. Biashara ya  Papa Wali imevurugika jambo linalomlazimu Latifa kuchangia katika shughuli za kila siku za  kuyakimu  mahitaji ya familia. Wazazi wake Latifa nao hawajui kusoma na kuandika na wanalazimika kuzitathmini athari za kutomsomesha binti yao.Jee,mchango na ushawishi wa Kakake Elinam na rafikiye Zakia utaweza kuwa chachu ya mabadiliko? Ipi hatma ya Epiphane, mfanyakazi wa Papa Wali asiyejua kusoma na kuandika?    
Michezo ya Noa Bongo:Jenga Maisha yako  inaweza kusikilizwa katika lugha sita tofauti: Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kihausa, Kireno  na Kihabeshi. Mradi  huu unaungwa mkono na Wizara ya Mambo ya   Nje ya Ujerumani
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi