Wajumbe wa SADC mkutanoni |
Taarifa hiyo Iliyotolewa jana kwenye mkutano wa kilele wa SADC nchini Namibia na kuhudhuriwa na Rais wa DRC Joseph Kabila,imezitaka nchi jirani kuchangia harakati za kuleta amani , usalama na utulivu nchini DRC.
Askari wa DRC wakisaidiwa na kikosi maalumu cha askari wa umoja wa mataifa UN walianzisha mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa M23 mwezi uliopita katika eneo la Mashariki mwa DRC.
SADC pia ilivipongeza vikosi vya askari wa serikali ya DRC na kikosi maalum cha umoja wa mataifa UN kwa kuendelea kutoa shinikizo la kijeshi kwa waasi wa M23 na makundi hasi mengine mMashariki mwa DRC
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!