Shahidi wa kwanza kutoka upande wa mashtaka, amefika
mbele ya mahakama ya kimataifa ICC kutoa ushahidi dhidi ya naibu Rais wa
Kenya William Ruto.
Mahakama inamlinda shahidi huyo kwa kutoonyosha sura yake.Shahidi alianza kwa kuahidi kusema ukweli. Alielezea ambavyo familia yake ilijiunga na mamia ya watu wa kabila la Kikuyu wakiwa na magodoro yao pamoja na blanketi.
Walikuwa wanatafuta hifadhi katika kanisa la Assemblies of God church katika kijiji cha Kiambaa karibu na mji wa Eldoret ambalo liliteketezwa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini waliokuwa wamekimbilia usalama wao.
Hii ilikuwa baada ya wenyeji wa kabila la Kalenjin kuwaonya kuwa wangeadhibiwa vikali ikiwa wangekosa kupigia kura chama cha kisiasa cha ODM kinachoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.
Shahidi huyo anatoa ushahidi wake akiwa nyuma ya kitambaa cha dirisha ndani ya mahakama huku kwenye TV sura yake ikiwa imezuiwa kuonekana ili kulinda usalama wake.
Naibu Rais William Ruto naye alitizama kutoka upande wa kushoto lakini sura yake imebanwa kabisa, hawezi kuonekana,.
Ushahidi wake unagusia siku ya tarehe mosi mwezi Januari. Aliambia mahakama kuwa maelfu ya watu walikuwa wanakuja kuizingira kanisa hiyo wakiimba huku wakiwa wamefunika nyuso zao kwa matope, wengi walikuwa wanavalia vitambaa kwenye vichwa vyao.
Alisema kuwa walikuwa wamjihami kwa mapanga na sil
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!