Kongamano hilo ambalo huratibiwa na kampuni ya Soccerex kitakuwa na dhumuni ya kutoa semina ya kuzitambua fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo ndani ya mchezo wa soka na namna ya kuzitumia katika kuhakikisha bara la Afrika linanufaika vizuri na mchezo huo wenye utajiri na ufuasi mkubwa duniani.
Kongamano hilo ambalo litaanza tarehe mosi Oktoba mpaka tarehe 2 mwezi huo mwaka huu, katika uwanja wa Moses Mabhida, litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya soka Afrika, vilabu na viongozi wa kiserikali wanashughulikia michezo katika nchi husika.
Tanzania mpaka sasa ina uwakilishi wa watu watatu akiwemo Naibu waziri wa habari, utamaduni, na michezo Amos Makalla atayemuwakilisha waziri Fenella Mukangara, pia aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kaburu na wakala wa kimataifa Damas Ndumbaro.
Mgeni rasmi katika kuongamano hilo la siku mbili atakuwa Mr.David Dein, makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Arsenal na Chama cha soka cha England.
Kongamano hili linatagemewa kuhudhuriwa na wadau wa soka wapatao 1,000 kutoka ulimwenguni kote.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!