MWENYEKITI wa kamati ya
afya ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Michel D’Hooghe ameshauri kuwa
michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 ni lazima
ichezwe katika majira ya baridi. D’Hooghe
amesema anajua Qatar wana uwezo wa kuandaa michuano hiyo katika majira
ya kiangazi ambapo timu zinaweza kufanya mazoezi na kucheza katika hali
ya hewa inayokubalika lakini tatizo linabaki kwa mashabiki watakaokwenda
kushuhudia michuano hiyo. Amesema
mashabiki watahitaji kusafiri kutoka uwanja mmoja kwenda mwingine na
anafikiri itakuwa sio vyema kwao kufanya hivyo katika sehemu yenye joto
linalozidi nyuzi joto 47 au zaidi. Tayari
rais wa FIFA Sepp Blatter amekubaliana na mpango wa kuangalia uwezekano
wa kubadilisha michuano hiyo kutoka katika majira ya kiangazi kama
ilivyozoeleka kwenda majira ya baridi. Lakini
mpango huo wa kuhamisha michuano hiyo kati ya Novemba na Desemba 2022
unapingwa vikali na Uingereza ambao wanalalamika utavuruga ratiba ya
ligi yao.
Home »
michezo ulaya
» TIMU YA MADAKTARI WA FIFA YASHAURI KOMBE LA DUNIA 2022 NCHINI QATAR LIFANYIKE MAJIRA YA BARIDI.
TIMU YA MADAKTARI WA FIFA YASHAURI KOMBE LA DUNIA 2022 NCHINI QATAR LIFANYIKE MAJIRA YA BARIDI.
Written By Unknown on Tuesday, 17 September 2013 | Tuesday, September 17, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!