Siasa haihusiani tu na bunge na serikali. Ushiriki katika siasa huanzia
nyumbani! Hata kubadilisha kitu katika eneo mtu analoishi kunaweza
kuleta mageuzi makubwa.
Ushiriki wa kisiasa unavuka mipaka ya kupiga kura kwenye chaguzi
Kupitia vipindi vyake kuhusu masuala ya familia - jinsi ya kuwa mshiriki
katika kisiasa mradi wa Learning by Ear - Noa Bongo Jenga Maisha Yako
unawaeleza wasikilizaji wake kuhusu maisha ya kila siku ya familia ya
kiafrika na kuonyesha jinsi maamuzi ya kisiasa yanavyopitishwa hata
katika maisha ya kila siku. V
ipindi hivi vinafuatilia maisha ya ndugu watatu wanaofuatilia kutimiza ndoto zao bianfsi. Betty, aliye wa mwisho, ni muimbaji mwenye kipaji anayetaka kuunda kwanya shuleni. Ronnie ana ari ya kuwa mchezaji kandanda na anataka kuwa kapteni wa timu yake. Eveline, ambaye ndiye mkubwa wao, amemaliza tu masomo yake ya shule ya sekondari na angependa kuwa diwani.
Kuelewa mchakato wa kijamii na kisiasa
Katika jitihada zao, ndugu hawa watatu wanalazimika kukabiliana na vikwazo mbalimbali. Matatizo haya yanahusiana na kanuni maalum na kijamii na kisiasa kama vile uongozi, ufisadi, kujenga miungano, kuripoti habari na vyama vya kisiasa. Sio mipango yote ya vijana hawa chipukizi ambayo inafaulu, lakini Betty, Ronnie na Eveline wanajifunza kutokana na makosa yao wenyewe. Juu ya yote hayo, washirika wachanga kisiasa wanaanza kuelewa mambo mengi kuhusu maana ya ushiriki wa kisiasa katika maisha halisi.
Vipindi vya “Learning by Ear” ‘ Noa bongo Jenga Maisha yako’ vinasikika katika lugha sita; Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Amharic. Na kufadhiliwa na wizara ya nchi za kigeni ya Ujerumani

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!