MSHAMBULIAJI Robin van Persie anataka
kuongeza mkataba wa kuichezea Manchester United ndani ya miaka yake
mitatu ilyobaki katika Mkataba wake wa sasa.
Van Persie alikuwa na mwanzo mzuri
katika msimu wake wa kwanza Old Trafford, akitwaa kiatu cha dhahabu cha
Ligi Kuu England kwa mara ya pili mfululizo na kuiwezesha United kutwaa
taji Barclays.
Inamaanisha Mholanzi huyo hakukosea kuondoka Arsenal na kuhamia kwa wapinzani wao wao.
VIDEO Kaangalie Manchester United wakifanya mazoezi kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa
Mholanzi matawi ya juu: Van Persie (wa pili kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga dhidi ya Crystal Palace Jumamosi |
Akizungumza na mshindi wa zamani wa
Kombe la Ulaya na United, Paddy Crerand katika mahojiano maalum ya
Televisheni ya klabu hiyo, MUTV, Van Persie alisema anataka kuendelea kuichezea zaidi klabu hiyo.
"Nina mika mitatu zaidi mbele,
ningependa kukaa zaidi,"alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
"Nafahamu, na ninaona watu walionizunguka, kufanya maamuzi ambayo
nafikiri hao watu wanaweza kugeuka na kusema; "Yalikuwa ni mazuri?".
Sitaki hivyo.
"Nataka kucheza muda mrefu kadiri inavyowezekana katika kiwango cha juu,".
Kushinda mataji ndio kitu kinachomvutia
zaidi Van Persie, ambaye hakuwahi kushinda chochote akiwa Arsenal tangu
walipotwaa Kombe la FA kwa kuifunga United kwenye Fainali mwaka 2005.
Bingwa: Van Persie akisherehekea kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, Mei mwaka huu |
Tayari ameongeza taji la Ngao ya Jamii
katika kabati lake baada ya ubingwa wa Ligi Kuu na ana matumaini ya
kunyanyua mataji zaidi United.
"Hiyo (kushinda mataji) ndiyo mpango
mzima,"alisema. "Mwaka jana tulipata taji moja kati ya manne. Sasa
tunatakiwa kutazama hili katika upande mwingine.
"Tuna nafasi ya kupata matano mwaka huu.
Mangapi tutabeba kati ya hayo matano? Kwa mtazamo wangu tutakuwa tayari
kushinda mawili au matatu.'
Baada ya mechi mbili bila ushindi wala
bao, United walirejea kwenye furaha ya ushindi katika Ligi Kuu England
mwishoni mwa wiki, huku Van Persie akifunga bao lake la tano msimu huu
katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace waliomaliza 10.
Endelea: Van Persie alitua United msimu uliopita kutoka Arsenal |
Sasa Mashetani Wekundu wanaingia katika
mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa katika zama za David Moyes,
wakimenyana na Bayer Leverkusen usiku wa leo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!