Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin |
Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican,
Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na
mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na
Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone
amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati
akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.
Hata hivyo, msimamo huo unaweza kupingwa na
waumini wengi wenye misimamo mikali ndani ya kanisa hilo ambao bado
wanaamini kuwa kuishi useja ndiyo mfumo na utamaduni unaofaa ndani ya
kanisa hilo.
Kwa upande wake, Papa Francis mwaka jana hata
kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alizungumzia suala hilo kwa
maneno mafupi kuwa angependa kuona mfumo huo ukibaki kama ulivyo.
Msimamo huo wa Askofu Mkuu Parolin unamaanisha
kuwa kuna haja ya kanisa hilo kufanya mabadiliko makubwa kwenye kanuni
ngumu ya useja kwa mapadri wake.
“Useja si suala la kitaasisi, lakini linaonekana
kuwa kweli, linaaminika. Ni suala gumu ambalo linaweza kujadiliwa kwani
si imani ya kanisa (dogma), halihusu imani ya kanisa,” alisema Askofu
Mkuu Parolin.
Askofu huyo alisema kwa kuwa siyo suala la kiimani, useja katika kanisa hilo limezama zaidi kwenye utamaduni.
“Juhudi za kanisa kuendelea na mfumo huo, hazina
budi kufanyika, pia zisizuie mjadala,” alisema na kuongeza: “Hakuna
anayeweza kuzuia mjadala huu kwa maelezo kuwa ni suala ambalo limepitwa
na wakati.”
Akiwa Waziri Vatican, Askofu Mkuu Parolin
anaonekana kwa wengi kama mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa baada ya
Papa Francis tofauti na watangulizi wengi wa kiongozi huyo wa Kanisa
Katoliki duniani ambao kwa miaka mingi wamekuwa na msimamo kwamba jambo
hilo halifai kujadiliwa.
“Kumekuwa na upinzani mkubwa kwenye mjadala huu wa
useja,” anasema Mhariri Mtandao na Mhariri wa zamani wa Gazeti la
Kikatoliki la Uingereza, The Tablet, Abigal Frymann na kuongeza: “Mawazo
haya ya Parolin yatazusha mjadala mkubwa.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!