Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Wakuu wa dini wa Somalia wailaani al-Shabaab, watoa njia mpya dhidi ya msimamo mkali

Wakuu wa dini wa Somalia wailaani al-Shabaab, watoa njia mpya dhidi ya msimamo mkali

Written By Unknown on Monday, 16 September 2013 | Monday, September 16, 2013

Mjumbe akisoma Korani kabla ya Mkutano wa Taifa wa Kukabiliana na Suala la Msimamo Mkali nchini Somalia. Katika taarifa rasmi ya mwisho ya mkutano, ujumbe ulitoa fatwa ya vipengele saba dhidi ya al-Shabaab. [Stuart Price/AU-UN IST/AFP]Viongozi wa dini wa Somalia waliungana pamoja katika onyesho la pamoja ambalo halijawahi kutokea siku ya Jumatano (tarehe 11 Septemba), wakitoa fatwa ya shutuma dhidi ya al-Shabaab na kutoa njia mpya dhidi ya itikadi za wenye msimamo mkali ambazo zinatishia mustakabali wa Somalia.
Kuanzia tarehe 7 hadi 11 Septemba, ujumbe wa wahubiri wa dini zaidi ya 160 na wataalamu wa dini kutoka kote nchini na nje ya nchi walikutana katika Hoteli ya Jazeera huko Mogadishu ili kushiriki katika Mkutano wa Kitaifa wa Kukabiliana na Suala la Msimamo Mkali nchini Somalia. Mkutano huo, ambao uliitishwa na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ulilenga kuwezesha majadiliano ya kina kuhusu msimamo mkali katika nchi na kuandaa mpango wa taifa wa kina kupambana na al-Shabaab.

Kuungana dhidi ya al-Shabaab

Mwishoni mwa mkutano, wajumbe walikubaliana kuwa na mshikamano katika mapambano dhidi ya msimamo mkali, kusaidia serikali utekelezaji wa sharia kama ilivyoidhinishwa na bunge la the Somalia mwaka 2009 na kamwe kutovumilia mauaji ya kiholela ya Wasomali yanayofanywa na al-Shabaab, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya mwisho.
Wajumbe pia walikubaliana kwamba itikadi ya al-Shabaab haina msingi katika imani ya Kiislamu, bali inachochewa na tamaa ya kupata madaraka kwa kutumia nguvu kupitia aina ya utawala wa kidikteta na kuchukua mali za watu isivyo halali.
Wakuu wa dini hao walisema vitendo vya al-Shabaab vinalenga kuwashinda wananchi wa Somalia na kuharibu imani yao, utamaduni na utaifa.
"Al-Shabaab wanaleta tishio la taifa kwa amani, maendeleo, na utulivu katika Somalia," taarifa rasmi ilisema. "Kuunga mkono na kuimarisha serikali ya Somalia ni njia bora ya kupambana na unyanyasaji wa al-Shabaab dhidi ya Somalia na wananchi wake, na hivyo, litakuwa jukumu la serikali ya shirikisho ya Somalia, uongozi wa mikoa mbalimbali, na umma wa Somalia kuungana pamoja katika kuimarisha na kulinda maadili ya kizalendo."
Wajumbe pia bila kwa pamoja walitoa vipengele saba vifuatazo vya fatwa:
1. "Al-Shabaab imepoteza mwelekeo wake na inawaongoza wananchi wa Somalia katika njia isiyo sahihi. Itikadi wanayoieneza ni hatari kwa Uislamu na kuwepo kwa jamii ya Kiislamu."
2. "Serikali ya Somalia ni serikali ya Kiislamu na inakataza kupigana dhidi ya [wanachama wake] au kuwachukulia kama sio Waislamu."
3. "Kikundi cha al-Shabaab chenye siasa kali lazima kitubu kwa Mungu kwa itikadi zao za kupotosha na vitendo vya uhalifu vya kutisha."
4. "Inakatazwa kujiunga na al-Shabaab au kutoa kwao aina yoyote ya msaada."
5. "Ni dhambi kutoa malazi kwa wanachama wa al-Shabaab. Ni jukumu la dini kuwakabidhi wanachama wa al-Shabaab kwa taasisi za usalama ya serikali ya Somalia."
6. "Ni dhambi kupatana kwa niaba ya wanachama wa al-Shabaab walio mikononi mwa taasisi za usalama za serikali."
7. "Viongozi wa Somalia wana jukumu la kidini la kuulinda umma wa Somalia kutokana na al-Shabaab, vivyo hivyo, raia wa Somalia wana wajibu wa kuisaidia serikali katika operesheni yake dhidi al-Shabaab."

Mapendekezo

Washiriki wa mkutano walitaja mapendekezo yanayohusiana na mada kuu tano: kuimarisha usalama, kujenga utulivu wa kisiasa, kuendeleza ukuaji uchumi, kuimarisha mfumo wa sheria na kuuelimisha umma kuhusu msimamo mkali.
Mapendekezo ya usalama yanajumuisha kujenga uwezo wa vikosi vya usalama, kuimarisha ushirikiano na ubia kati ya polisi na wananchi, na kuimarisha ushirikiano na washirika wa jumuiya ya kimataifa ili kuwakamata magaidi.
Ili kujenga utulivu wa kisiasa, wajumbe walipendekeza serikali kurudisha maadili ya kizalendo, kuweka wazi mawasiliano baina ya umma, serikali na viongozi wa dini ili kutunza amani na kuimarisha usulihishi na kutoa programu za urekebishaji tabia kwa wanachama wa al-Shabaab ambao bado hawajawa na msimamo mkali kikamilifu.
Wajumbe walipendekeza serikali itunge sheria inayopiga marufuku ufadhili wa vikundi vyenye msimamo mkali, kujenga mazingira mazuri ya ukuaji wa uchumi huku pia ikiimarisha ushirikiano kati ya taasisi za ulinzi na jumuiya ya wafanyabiashara, na kuunda mfuko kwa ajili ya urekebishaji tabia za wanachama wa al-Shabaab.
Haki lazima ilindwe ili kuendeleza umoja na kulinda usalama wa taifa, wajumbe walisema.
Wakuu wa dini pia walipendekeza kwamba serikali itoe mafunzo kwa shule na walimu wa dini ili kuwaandaa ipasavyo wanafunzi, kuwafanya wasiathirike sana na kuwa na siasa kali.
Mkutano ulifungwa kwa kutoa wito kwa serikali kuanzisha shirika la taifa la kupambana na kusambaa kwa itikadi ya msimamo mkali nchini Somalia ndani ya siku 30, na kuandaa mkutano wa kufuatilia kati ya Somalia na Wanazuoni wa kiislamu wa kimataifa ndani ya siku 90.

Hatua ya kihistoria dhidi ya misimamo mikali

Hii ni mara ya kwanza uwakilishi wa wakuu wa dini maarufu wa Somalia kutoa kauli ya pamoja dhidi ya al-Shabaab na kwa pamoja kuiunga mkono serikali katika mapambano yake dhidi ya ugaidi, alisema Omar Sheikh Abdirahman, mkurugenzi wa Kituo cha Usuluhishi na Mazungumzo mjini Mogadishu.
Fatwa waliyotoa itawahamasisha Wasomali kutathmini na kufikiria upya mawazo yao kuhusu siasa kali, ambayo itaharakisha kushindwa kwa al-Shabaab's defeat, Abdirahman aliiambia Sabahi.
"Watu wengi ambao kwa sasa wanafikiri kwamba al-Shabaab wako katika njia sahihi watashawishika kuwa hawakuwa sahihi," alisema, na kuongeza kwamba kupinga kwa nguvu zote uungaji mkono kwa al-Shabaab kutasababisha wafuasi wao wengi kubadili mawazo yao.
Sheikh Hassan Jami Mohamud, Imamu katika Taasisi ya Daawah ya Minnesota huko Saint Paul, Minnesota, ambaye alisafiri kuja Mogadishu kushiriki katika mkutano huo, alisema kwamba mafanikio makubwa zaidi ya kongamano lilikuwa ni kuwasaidia Wasomali kuamua hatima yao wenyewe. Katika jitihada hizo, ni muhimu sana, alisema, kwa wakuu wa dini, serikali na umma kushirikiana katika vita dhidi ya al-Shabaab.
"Ni muhimu kwamba sote tunaungana dhidi ya watu wanaoua wananchi wasio na hatia […] kwa itikadi potofu ambayo haina msingi katika dini ya Kiislamu," aliiambia Sabahi.
Mohamud alisema utekelezwaji wa mafanikio wa mapendekezo yote kutahitaji juhudi za uungwaji mkono kutoka kwa wadau huku serikali ikiwa inaongoza njia.
Hata hivyo, alisema, mapendekezo yanayohusu usalama yanatakiwa kupewa kipaumbele. "Serikali lazima iweke upande kazi nyingine na kuandaa mpango wa usalama kwa sababu bado kuna hofu ya milipuko mengine ambayo itaua watu wengi zaidi," alisema.
Licha ya mapokezi chanya kwa jumla, mwenyekiti wa Ahlu Sunna wal Jamaa Sheikh Omar Abdulkadir alikosoa tukio hilo kwa kusema kwamba halikuwa linawakilisha wakuu wote wa dini.
"Hatukuarifiwa wala kualikwa," aliiambia Sabahi.
Kwa kuongezea, alisema kwamba baadhi ya wakuu wa dini waliohudhuria katika kongamano walikuwa waungaji mkono wa al-Shabaab hapo kabla. "Mtu ambaye jana aliwashawishi watu wafanye ulipuaji na kukata watu vichwa hawezi kuwashawishi vyenginevyo leo," alisema.
Mohamud alijibu kwa kusema kwamba vikundi mbali mbali vya wakuu wadini wa Somalia vilihudhuria kongamano. na makongamano ya siku za mbele yatashighulikia malalamiko mengine yoyote.

Kushinda vita vya itikadi

Alas Haji Ahmed, mwanafunzi wa biashara mwenye umri wa miaka 32 katika Chuo Kikuu cha SIMAD mjini Mogadishu, alisema alikaribisha mapendekezo na fatwa ya wakuu wa dini lakini alisema ilikuwa imechelewa sana.
"Nilitamani [wakuu wa dini] wangeyatoa muda mrefu uliopita kwa vile al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kigaidi katika nchi nzima kwa muda mrefu," aliiambia Sabahi.
Njia pekee ya kushinda vita dhidi ya al-Shabaab ni kwa wakuu wa dini kuuelimisha umma juu ya itikadi yao potofu, Ahmed alisema.
"Tatizo limekuwa ni umma ulioelimishwa vibaya. Tuanchokitaka kutoka kwa wanazuoni ni kufanya mihadhara mfululizo katika wilaya zote za Mogadishu ili umma uweze kujifunza kwamba njia potofu ambayo al-Shabaab wanatumia dini haihusiani na misingi ya Kiislamu," alisema.
Roble Dahir, mwanafunzi wa uandishi wa habari mwenye umri wa miaka 28 katika Chuo Kikuu cha Mogadishu, alisema kwamba vita dhidi ya al-Shabaab vilikuwwa vita vya kiitikadi.
"Ni jambo zuri sana kuona kwa mara ya kwanza wakuu wa dini wanazungumza kwa sauti moja dhidi ya itikadi ya al-Shabaab, "Serikali inapaswa kuweka vipaza sauti kwanye sehemu za umma kuwaambia watu kile ambacho Uislamu unasema kuhusu milipuko ambayo al-Shabaab wanafanya inayoua wananchi."
Alisema kuwa ulinzi maalumu unapaswa kutolewa kwa wakuu wa dini wakati wanapokwenda misikitini kutoa mawaidha yao kwa vile al-Shabaab imejulikana kwa kuwalenga wahanga ndani na nje ya misikiti.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi