Mwezi mmoja baada ya shambulio la kigaidi katika jumba la
kibiashara nchini Kenya la Westgate ambalo kundi la Alshabab
lilijigamba kuhusika, hofu ya kutokea mashambuli okama hayo imeongezeka
katika ukanda wa Afrika Mashariki hususan nchini Uganda ambako polisi
imewatolea wito wananchi kuwa makini.Polisi nchini Uganda kupitia
mtandao wake wa kijamii imetowa taarifa ya kuwataka wananchi wa taifa
hilo kuwa makini katika shguhuli zao za kila siku kufuatia kitisho cha
kutokea kwa shambulio la kigaidi.
Ujumbe huo wa tahadhara unatokea baada ya ujumbe wa onyo
uliotoolewa na Marekani jana siku ya alhamisi. Balozi wa Marekani jijini
Kampala aliomya kwamba jijini humo kunaweza kutokea shambulio kama lile
la Westgate.Hata hivyo, ubalozi huo haukutowa maelezo zaidi kuhusu lini na wapi litapotokea shambulio hilo. Katika barabara za Kampala, usalama umeimarishwa.
Katika moja miongoni mwa vituo vya kibiashara jijini Kampala la
Garden City, magari mengi yameshuhudiwa yakifanyiwa ukaguzi kabla ya
kuingia sehemu hiyo, huku kila anaingia lazima afanyiwe ukaguzi wa hali
ya juu. Polisi wameshuhudiwa wakipiga doria huku wakijizaiti vya kutosha
na silaha.Takriban watu 67 walipoteza maisha katika tukio la Westgate mwishoni mwa mwezi Septemba, shambulio ambalo liliendeshwa na kundi la Al shabab lililojigamba kulipiza kisase kufuatia majeshi ya Kenya kuendesha operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Al Shabab tangu mwishoni mwa mwaka 2011.
Majeshi ya kenya yaliingia nchini humo yakiwa pekeake, kabla ya
kujiunga na kikosi cha Afrika cha kulinda amani nchini Somalia AMISOM
kilichotumwa nchini humo tangu mwaka 2007 kulisaidia jeshi dhaifu la
Somalia katika vita dhidi ya wanamgambo wa al Shabab na ambapo nchi za
Uganda na Burundi ndizo zilizojitokeza na kuwa kwenye mstari kwa kwanza
katika kutuma wanajeshi wake nchini humo.Nchi ya Uganda imekuwa kitisho mara kadhaa cha mashambulizi ya kundi la Al Shabab na ambapo mashambulizi kadhaa yameripotiwa nchini humo. Watu 76 walipoteza maisha jijini Kampala katika shambulio la kujitowa muhanga lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabab wakati wa fainali la kombe la dunia.
Tangu kutokea kwa shambulio la Westgate, nchi ya Burundi imekuwa
ikitishiwa pia na kundi la Al Shabab na ambayo imekuwa ikitahdharishwa
na Marekani, imezidisha ulinzi na usalama wakati Warundi wakihofia kuwa
kwenye orodha itayofuata kushambuliw ana wanamgambo hao na ambo wamenaza
kuitaka serikali ya nchi hiyo kuyaondowa majeshi yake nchini Somalia.Onyo hiyo ya polisi wa Uganda inakuja wakati huu kukiwa na taarifa kuhusu kumtambuwa mmoja miongoni mwa magaidi walitekeleza shambulio la Westgate baada ya kuonekana kwenye camera za usalama na kutambulika kuwa ni Hassan Abdi Dhuhulow kijana mwenye umri wa miaka 23 raia wa Norway mwenye asili ya Somalia ambaye aliondoka nchin humo akiwa bado mdogo.
Ndugu wa kijana huyo ambaye alihojiwa na kituo cha runinga ya Norway,
alikanusha kuwa mtu huyo sio ndugu yake. Takriban mwezi mmoja baada ya
kutokea shambulio hilo swala kubwa lililopo ni kuwatambua washambuliaji.Mbali na watu 67 waliopoteza maisha katika tukio hilo la Westgate, shirika la msalaba mwekundu limeorodhesha idadi ya watu 23 waliopotea katika shambulio hilo.
Hapo jana polisi nchini Kenya imefahamisha kwamba imegundua fuvu katika vifusi kwenye jengo hilo la Wesgate na vipimo vinafanyika kujuwa ni nani.


0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!