Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Baada ya Irene Uwoya kuweka kituko cha aina yake jana, soma hiki kingine tulichokipata leo

Baada ya Irene Uwoya kuweka kituko cha aina yake jana, soma hiki kingine tulichokipata leo

Written By Unknown on Saturday, 12 October 2013 | Saturday, October 12, 2013



Juzi mwanadada Irene Uwoya aliwavunja mbavu wadau mbalimbali wa filamu nchini Tanzania baada ya kuweka picha (Inayoonekana pichani)  ya moja ya scenes za filamu yake mpya ambayo bado hatujapata jina lake ikumuonesha jambazi  (aliyepewa jina la “JAMBAZI MSTAARABU” na fans wa filamu )akimtishia Irene Uwoya bastola kama anataka kumuua hivi.
Jambazi huyo ambaye kwanza anaonekana “Sharobaro” na akifanya uhalifu kistaarabu kwa kuvua viatu “eti asije akachafua nyumba anayoiba” huku wananchi wengine wakiongezea kuwa Jambaz ana mzuka wa kuiba mpaka viatu kavua,
Baada ya picha hiyo kupondwa sana na wadau jana mdau wetu mmoja  ameamua kututumia kioja kingine alichowahi kukutano nacho kwenye filamu hizi za bongo.
Mdau anasema japokuwa hakumbuki jina la filamu hiyo vizuri anakumbuka scene moja ya kwenye filamu hiyo ambayo kulikuwa na jini mmoja aliyetumwa akamuue dada mmoja katika filamu hiyo.
Haya chini ndio maneno ya mdau wetu huyu, yote hii ni katika kuboresha filamu zetu na sio kuziponda.
“Kuna cku nlikua home siriaz nacheki Bongo muvi... Nmevumilia kinoma najifanya mzalendo... Sasa filamu ilikua ina jini moja katili sana... Limetumwa likamuue maza mmoja na ndugu... Sasa likawa linavuka bara bara eti...taratibu nikaona linajisogeza kwenye zebra cross  huku likiangalia kushoto na kulia before halijavuka..jini gani sasa hili? Sio kwamba linatakiwa livuke tuu? Mi sijawai kusikia jinni likiogopa kugongwa na gari.. .Nlimind sana..”
Dah, kwa mwendo huu itabidi tujipange sana yani, ni hayo tuu!
USHAURI: Tujaribu kutengeneza uhusika halisi ndani ya filamu sio bora liende.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi