SHIRIKISHO la Soka
Duniani-FIFA limebainisha kuwa kampuni ya GoalControl ya Ujerumani ndio
itakayofunga kamera za mfumo wa teknologia ya kompyuta katika goli
katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil na Kombe la Klabu
Bingwa ya Dunia itakayofanyika nchini Morocco mwaka huu. Katika
taarifa iliyotumwa katika mtandao wake FIFA imedai kuwa mfumo huo
ulifanyiwa majaribio katika michuano ya Kombe la Shirikisho mapema mwaka
huu baada ya kampuni hiyo kushinda zabuni. Taarifa
hiyo iliendelea kudai kuwa kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika
majaribio ya mfumo huo kwenye Kombe la Shirikisho FIFA inathibitisha
kuwa GoalControl ndio watapewa jukumu ya kufunga vyombo vinavyotumia
mfumo huo kwenye michuano hiyo. Mfumo
wa GoalControl unatumia kamera 14 zenye uwezo wa hali ya juu zinafungwa
pembezoni kwa milingoti ya goli ili kuhakiki kama mpira umevuka mstari
au la.
Home »
michezo ulaya
» FIFA YAWAPA TENDA WAJERUMANI KUFUNGA GOAL-LINE SYSTEM KWENYE KOMBE LA DUNIA BRAZIL.
FIFA YAWAPA TENDA WAJERUMANI KUFUNGA GOAL-LINE SYSTEM KWENYE KOMBE LA DUNIA BRAZIL.
Written By Unknown on Friday, 11 October 2013 | Friday, October 11, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!