Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HAWA NDO MAKIPA WANAO KUJA JUU KWA KULIPWA MKWANJA MREFU ULAYA

HAWA NDO MAKIPA WANAO KUJA JUU KWA KULIPWA MKWANJA MREFU ULAYA

Written By Unknown on Thursday, 17 October 2013 | Thursday, October 17, 2013

SUPASTAA Mreno, Cristiano Ronaldo, ni mwanasoka anayelipwa fedha nyingi duniani kwa sasa. Staa huyo anapokea Pauni 15 milioni kwa mwaka baada ya makato ya kodi na kabla ya malipo ya bonasi nyingine.
Mshahara wake kwa wiki ni Pauni 288,000 akimwacha kwa mbali mwanasoka aliyesajiliwa kwa uhamisho ghali zaidi duniani kwa sasa, Gareth Bale ambaye analipwa Pauni 8.3 milioni kwa mwaka.
Lakini, mara nyingi imekuwa ikisikika juu ya wachezaji wa nafasi nyingine wakiongoza kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi na kulipwa mishahara mikubwa, lakini si makipa. Ushawahi kufikiria ni kipa gani analipwa fedha nyingi kwa sasa?
Makala hii inazungumzia makipa wanaolipwa fedha nyingi kwa mwaka katika klabu zao na kuweka rekodi. Achana na makipa kama Joe Hart, David De Gea, Pepe Reina, Hugo Iloris na Salvatore Sirigu, kuna makipa watano bora wanaovuta mshiko wa nguvu.
5. Victor Valdes - Barcelona
Kipa huyo Mhispaniola ambaye hivi karibuni alisema ataihama Barcelona mwishoni mwa msimu pale mkataba wake utakapofika tamati, ni miongoni mwa makipa wanaolipwa pesa nyingi katika klabu zao.
Valdes yumo kwenye tano bora. Kwa mwaka anavuta Pauni 5 milioni kutokana na mkataba wake wa sasa anaoutumikia Nou Camp.
4. Petr Cech - Chelsea
Ni mmoja wa makipa mahiri kabisa katika Ligi Kuu England kwa muongo uliopita. Kwenye klabu ya Chelsea, kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech analipwa Pauni 5.2 milioni kwa mwaka.
3. Gianluigi Buffon - Juventus
Ni kipa aliyedumu kwenye kiwango bora kwa muda mrefu. Kwenye klabu ya Juventus, Buffon, anatazamwa kama nembo ya timu hiyo. Umahiri wake unamfanya kuwa kipa anayeingia mikataba minono inamfanya awemo kwenye orodha ya makipa wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwenye mchezo wa soka kwa sasa.
Buffon, ambaye kwa sasa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya Juventus ambayo ni bingwa wa Italia, analipwa Pauni 5.5 milioni kwa mwaka.

.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi