Abdullah al-Senussi |
Hatua hii ya ICC inaamanisha kuwa haitamtaka tena Senussi
kufika Hague na kumfunguliwa Mashtaka ya mauaji ya raia yanayomkabili
wakati wa mapambano kati ya majeshi ya serikali na waasi.
Mwaka 2011 Mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa na kufikishwa Hague kiongozi huyo wa zamani wa kitengo cha inteljensia nchini Libya baada ya kutoroka katika nchi yake.
Serikali ya Mauritania ilimkamata Sennusi na kumrudisha nchini Libya mwaka uliopita baada ya serikali ya mpito kipindi hicho kusema kuwa ilikuwa na uwezo wa kumfungulia mashtaka.
Hata hivyo, ICC imesema kuwa umauzi huo haushirikiani kwa vyovyote vile na kesi inayomkabili mwanaye Gaddafi , Saif al-Islam Gaddafi ambaye anatakiwa katika Mahakama hiyo ya Kimataifa ili kufunguliwa Mashtaka.
ICC inaitaka serikali ya Libya kumsafirisha Saif al-Islam Gaddafi mjini Hague kwa kile wanachosema kuwa katika Mahakama hiyo atapata haki lakini Serikali ya Libya inasisitiza kuwa ina uwezo wa kuhakikisha kuwa haki inatendeka.
Saif Gaddafi kwa sasa anashikiliwa katika mji wa Zintan Magharibi kwa nchi hiyo na wiki iliyopita waasi wanaomzuia walikataa kumfikisha Mahakamani jijini Tripoli wakati kesi ya Senussi ilipoanza.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!