Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Jeshi la AMISOM kuongezewa nguvu ya kupambana na wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia

Jeshi la AMISOM kuongezewa nguvu ya kupambana na wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia

Written By Unknown on Saturday, 12 October 2013 | Saturday, October 12, 2013


Wanajeshi wa AMISOM wakiwa nchini Somalia
Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU ulioanza hiyo jana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia umepitisha azimio la kuongeza idadi ya wanajeshi wanaopambana na wapiganaji wa kundi la Al-shabaab nchini Somalia, AMISOM.

Baraza la amani na usalama la AU limethibitisha kuwa AMISOM itaongezewa wanajeshi 6235 sawa na nyongeza ya asilimia 35 ili kuzidisha nguvu ya kulitokomeza kundi hilo lenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani wa Al Qaeda.
Ongezeko hilo litafanya idadi ya wanajeshi wa AU waliopo nchini Somalia kufikia 23,996.
Hata hivyo pendekezo hilo ni lazima liidhinishwe kwanza na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kabla ya wanajeshi hao kupelekwa Somalia.
Pendekezo hilo linakuja majuma kadhaa baada ya kutekelezwa kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya katika jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi, tukio ambalo kundi la Al-shabaab lilikiri kuhusika nalo kwa madai ya kuishinikiza Kenya iondoe wanajeshi wake nchini humo.
Majeshi ya AMISOM yapo nchini Somalia toka mwaka 2007 na yanaundwa na wanajeshi kutoka Kenya, Uganda na Burundi.
Mkutano wa AU unaoendelea mpaka hii leo utashuhudia mjadala wa swala la nchi za Afrika kujitoa kwenye mahakama ya ICC kwa madai kuwa mahakama hiyo imekuwa haiwatendei haki viongozi wa Afrika.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anaelekeo Addis Ababa kuhudhuria mkutano huo na yeye na Naibu wake William Rutto ni miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaokabiliwa na kesi katika mahakama hiyo.
Hata hivyo huenda kukashuhudiwa mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa nchi wanachama wa AU kwani baadhi ya nchi zinaonyesha dalili ya kutokubaliana na hoja ya bara la Afrika kujiondoa katika mkataba wa Roma.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi