Mama
ambaye mtoto wake wa kiume alifariki miaka 18 iliyopita amemuhifadhi
katika pombe na kuficha mwili wake kwenye sehemu ya chini ya makazi yake
ambako amekuwa akimhudumia muda wote tangu wakati huo... yote hayo ili
kijana wake aweze kuona anavyompenda.
Tsiuri
Kvaratskhelia ameuhifadhi mwili wa Joni Bakaradze uliozikwa ndani ya
jeneza la mbao sambamba na nyumba hiyo ya familia mjini Georgia,
mashariki mwa Ulaya.
Lakini
licha ya kuwa amekufa mwaka 1995, mwili wa kijana huyo mwenye miaka 22
umebaki ukiwa umekaushwa damu kikamilifu, shukrani kwa mama yake
aliyeonesha mapenzi ya kweli na uangalizi wa karibu.
Na kila
mwaka katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mama huyo amekuwa
akimbadilisha nguo - hadi miaka minne iliyopita pale uozo hatimaye
ulipofanya kazi hiyo kushindikana.
"Alitaka mtoto wake kumwona kwa namna hiyo," alielezea. "Naamini kutokea hapo mtoto huyo alianza kumpenda baba yake."
Pia
kuna dirisha dogo la kutazamia kwenye sehemu hiyo ya chini hivyo
familia, marafiki na wapita njia wanaweza kuona jinsi anavyoendelea.
Mama Kvaratskhelia amejifunza zaidi kuliko mbinu chache kumfanya mtoto wake huyo awe na mwonekano mzuri.
"Usiku
mmoja niliota pale sauti fulani iliponieleza kumshughulikia Joni kwa
kumwagia pombe hivyo kutokea hapo nimekuwa nikitumia mashuka yenye
unyevu yaliyozamishwa kwenye pombe kuhifadhi mwili wake," alisema.
"Hutakiwi kuuacha mwili huo bila mashuka hayo wakati wa usiku sababu
ngozi itabadilika na kuwa nyeusi kama makaa ya mawe."
Aliongeza:
"Kwa miaka 10 nimekuwa nikimbadilisha nguo zake wakati wa maadhimisho
ya siku yake ya kuzaliwa. Miaka minne tu iliyopita ndio sikuweza kufanya
hivyo.
"Alikuwa mtu safi, mume mwema, si kama hivi alivyo sasa."
Lakini
sasa Joni, ambaye sababu za kifo chake hazijafahamika, hatimaye anaanza
kuharibika tangu maradhi kumzuia Mama Kvaratskhelia kumpatia matunzo ya
kila siku anayohitaji.
"Nilikuwa naumwa hivi karibuni na sikuweza kuhudumia mwili wake," alisema. "Hiyo ilikuwa na athari kwake.
"Mtoto wangu ni anavutia. Nitakapoanza kutumia mashuka hayo ngozi yake itakuwa angavu tena na kila kitu kitakuwa kama kawaida."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!