Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Maandamano nchini Sudan ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta yachangia kulemaza shughuli za ukuaji wa uchumi

Maandamano nchini Sudan ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta yachangia kulemaza shughuli za ukuaji wa uchumi

Written By Unknown on Thursday, 3 October 2013 | Thursday, October 03, 2013

Waandamanaji nchini Suda wakipinga hatua ya Serikali kuongeza ruzuku kwenye mafuta iliyochangia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo
Waandamanaji nchini Suda wakipinga hatua ya Serikali kuongeza ruzuku kwenye mafuta iliyochangia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo

Wananchi wa Sudan wameendelea kufanya maandamano ya nchi nzima kushinikiza Serikali kusikiliza kilio chao cha kupunguza ruzuku kwenye mafuta kulikochangia kuongezwa kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.

Maelfu ya waandamanaji wameendelea kuonekana kwenye mitaa mbalimbali wakitaka Serikali kuondoa nyongeza ya ruzuku iliyochangia kupanda kwa bei ya mafuta kitu kinachoongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wa kawaida.
Jeshi la Polisi limeendelea kukabiliana na waandamanaji hao kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kitu kilichosababisha mamia ya raia kuendelea kujeruhiwa kwenye maandamano hayo.
Takwimu za serikali zinaonesha watu zaidi ya mia mbili wamejeruhiwa tangu kuanza kwa maandamano hayo huku watu thelathini na wanne wakifikwa na mauti japokuwa upinzani unasema zaidi ya watu hamsini ndiyo wameuawa.
Maandamano hayo yametajwa kama sehemu ya mkakati wa kuharibu uchumi wa Sudan kauli iliyotokewa na Rais Omar Hassan Ahmed Al Bashir aliyesema hawawezi kuondoa ruzuku hiyo kwani itasaidia kuimarisha uchumi wao.
Upinzani wenyewe umejiapiza kuendelea na maandamano hayo hadi pale ambapo Serikali itaondoa ruzuku hiyo wakiamini inalengo la kuendelea kuwanyonya wananchi wa kawaida wenye vipato vya chini.
Uingereza nayo imejitosa kuzungumzia maandamano hayo ambapo Katibu wa kudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje Simon Fraser amesema kile kinachoendelea nchini Sudan ni onyo kwa serikali na hivyo inafaa kuchukua hatua muafaka.
Fraser amesema ni lazima pande zote zilizopo kwenye mgogoro huo kukaa chini na kuangalia ni kwa namna gani tatizo hilo litamalizwa badala ya kuchochea na kuchangia umwagaji wa damu.
Mshauri huyo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague, Fraser alipata nafasi ya ,ukutana na Viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Karti na kumueleza navyoguswa kutokana na idadi kubwa ya waandamanji wanaoshikiliwa.
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani la Amnesty International kupitia Naibu Mkurugenzi wake kwa Afrika Lucy Freeman amesema kumekuwa na njama za serikali kuwakamata waandamanaji na kuwafungulia makosa wasiyotenda.
Waandamanaji wamefanya uharibufu mkubwa tangu kuanza kwa maandamano hayo ambapo vituo vya mafuta na magari yalichomwa moto huku maduka mengi yakishambuliwa, kuvunjwa na kuporwa bidhaa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi