Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor |
Awali kiongozi huyo aliwasilisha ombi katika mahakama ya mjini
Hague akitaka atumikie kifungo chake nchini Rwanda badala ya Uingereza
kama alivyopangiwa ili awe karibu na familia yake na kuwa na uhakika juu
ya usalama wake.
Hata hivyo ombi hilo limeonekana kutofua dafu kwani tayari amekwishawasili jijini London hii leo na hakuna taarifa zozote juu ya majibu ya ombi lake.
Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita ilimkuta Taylor na hatia ya kutenda makosa kumi na moja ya uhalifu wa kivita ikiwemo ugaidi, ubakaji, mauaji na matumizi ya watoto katika jeshi, kwenye machafuko ya zaidi ya miaka kumi nchini Sierra Leone ambapo watu zaidi ya elfu hamsini waliuawa.
Mnamo mwezi wa tisa Mahakimu katika mahakama maalumu nchini Sierra Leone SCSL walikataa rufaa ya Taylor dhidi ya hukumu yake ya awali rufaa ambayo haikutengua chochote.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!