WAKATI hatua ya kuwania kufuzu
Fainali za Kombe la Dunia 2014 ikiwa inakaribia kufikia ukingoni, kuna
hatihati ya mastaa mbalimbali kukosa fainali hizo.
Hadi wakati huu tayari nchi nyingine kutoka Ulaya,
Asia na Marekani ya Kusini zimeshafuzu kushiriki fainali hizo za soka
za dunia zitakazofanyika huko Brazil.
Nchi ambazo tayari zimeshafuzu ni Japan, Australia, Iran, Korea ya Kusini, Uholanzi, Italia, Argentina, Costa Rica na Marekani.
Hata hivyo, zipo nchi nyingi zenye majina makubwa
ambazo bado hazina uhakika wa kufuzu fainali hizo kwani zinatakiwa
kushinda mechi zao za mwisho au kukubali kuangalia Fainali za Kombe la
Dunia 2014 kwenye televisheni.
Timu hizo ambazo zipo kwenye hatihati ya kufuzu
zina mastaa wengi kama Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic, Javier
Hernandez, Luis Suarez na Cristiano Ronaldo.
England
Baada ya sare ya kutokufungana na Ukraine mwezi
uliopita, England bado inaongoza Kundi H katika makundi ya kuwania
kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2014 kutoka barani Ulaya (Uefa).
Katika Kundi H, mbali na England na Ukraine, timu
nyingine ni Montenegro, Poland, Moldova na San Marino. England inaongoza
kundi hili ikiwa na pointi 16 ikifuatiwa na Ukraine na Montenegro
ambazo zote zina pointi 15.
Kama katika mechi yao kesho Ijumaa England
itaichapa Montenegro halafu Poland ikaichapa Ukraine basi England
itafuzu Fainali za Kombe la Dunia, lakini kama England watashindwa
kufanya hivyo halafu Ukraine ikashinda basi mechi ya mwisho kati ya
England dhidi ya Poland itakuwa haina maana kwani Ukraine itakuwa
ikicheza mechi ya mwisho na San Marino ambayo katika kundi hili haina
hata pointi moja.
Ni wazi kama England itashindwa kufuzu, mastaa
kama Wayne Rooney, Steven Gerrard, Daniel Sturridge, Theo Walcott, Frank
Lampard, Jack Milner na wengine wengi hawatacheza Kombe la Dunia.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!