CHAMA cha soka cha
Misri-EFA kimelihakikishia Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwa wameweka
ulinzi wa uhakika katika mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia hatua ya
mtoano dhidi ya Ghana. Ghana
iliandika barua FIFA kuomba mchezo wao huo kuhamishwa na kuchezwa nje
ya Misri kutokana na matatizo ya kiusalama hivyo kuwafanya EFA kutoa
uhakika wa usalama katika mechi hiyo. Msemaji
wa EFA Azmy Megahed amesema tayari wamehakikishiwa usalama kutoka
wizara ya mambo ya ndani na jeshi la Misri hivyo hakuna kitu cha kuhofia
katika mchezop huo. Megahed
amesema mbali na kuhakikishiwa usalama lakini pia mchezo huo utachezwa
katika Uwanja wa El Defea El Gawe ambao unamilikiwa na jeshi la nchi
hiyo. Misri
itakwaana na Ghana Novemba 19 jijini Cairo katika mchezo wa mkondo wa
pili ya kufuzu michuano ya Kombe ya Kombe la Dunia huku mchezao wa
mkondo wa kwanza ukitarajiwa kuchezwa Jumanne katika Uwanja wa Baba Yara
jijini Kumasi.
Home »
michezo africa
» MISRI YAIHAKIKISHIA FIFA USALAMA WA KUTOSHA.
MISRI YAIHAKIKISHIA FIFA USALAMA WA KUTOSHA.
Written By Unknown on Monday, 14 October 2013 | Monday, October 14, 2013
Labels:
michezo africa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!