WAKATI kampeni za kufuzu
michuano ya Kombe la Dunia 2014 zikifikia hatua ya mwisho baadhi ya
timu mwishoni mwa wiki hii zinaweza kujihakikishia nafasi kushiriki
michuano hiyo mwakani. Wenyeji
Brazil tayari wameungana na wawakilishi kutoka bara la Asia ambao ni
Japan, Australia, Iran na Korea Kusini huku Ulaya tayari kukiwa na
vigogo Uholanzi na Italia pamoja na Marekani, Costa Rica na Argetina. Katika
siku chache zijazo timu zingine kutoka mataifa ya Afrika, Ulaya,
Amerika Kaskazini na Amerika Kusini nazo pia zinaweza kujihakikishia
nafasi katika michuano hiyo. Kwa
upande wa Ulaya nchi za Ubelgiji, Ujerumani, Switzerland, Urusi,
Bosnia-Herzegovina na Hispania zinaweza kujihakikishia nafasi ya kwenda
Brazil kama zikishinda michezo yao ya Ijumaa. Wakati
Upande wa Amerika Kusini nchi za Colombia, Chile, Uruguay na Ecuador
zote zinaweza kufuzu michuano hiyo kama wakishinda mechi zao, huku
Honduras nao wakiwa na uwezo wa kuwa nchi ya tatu kwa upande wa Concacaf
kufuzu michuano hiyo kama wakiifunga Costa Rica Ijumaa hii. Wikiendi
pia kutakuwa na mechi za mkondo wa kwanza za mtoano kwa uapnde wa
Afrika ambapo Burkina Faso wataonyeshana kazi na Algeria, Ivory Coast na
Senegal, Ethiopia na Nigeria, Tunisia dhidi ya Cameroon na Ghana
wataikaribisha Misri.
Home »
michezo ulaya
» NANI KUTANGULIA BRAZIL WIKIENDI HII?
NANI KUTANGULIA BRAZIL WIKIENDI HII?
Written By Unknown on Friday, 11 October 2013 | Friday, October 11, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!