MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund Robery Lewandowski ameweka wazi nia yake ya siku moja kucheza katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye mkataba wake na Dortmund unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alidai Septemba mwaka huu kwamba atasaini mkataba Bayern Munich Januari mwakani kabla ya kukanusha taarifa hizo baadae.
. |
Meneja
wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwa akimwinda
nyota huyo katika kipindi cha majira ya kiangazi lakini ilishindakana
baada ya Leandowski kuonyesha nia ya kwenda Bayern. Akihojiwa
Lewandowski amesema anaweza kusaini mkataba na klabu yoyote ifikapo
Januari lakini akakanusha kuwa hakuwahi kusema kwamba atasaini na
Bayern. Nyota
huyo aliendelea kudai kuwa kimetokea suala la kutoelewana na kukiri kuwa
ni kweli alifanya mazungumzo na Ferguson mwaka jana lakini
hawakuzungumzia masuala ya uhamisho.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!