Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Rais Kenyatta ataka kesi inayomkabili ICC kusitishwa

Rais Kenyatta ataka kesi inayomkabili ICC kusitishwa

Written By Unknown on Friday, 11 October 2013 | Friday, October 11, 2013

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa Hague
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya ICC kusitisha kesi ya uchochezi, ufadhili na kupanga machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2007 inayomkabili.

Kupitia kwa Mawakili wake, Kenyatta anasema anaamini kuwa haki haitapatikana katika Mahakama hiyo kwa sababu Mashahidi dhidi yake wameshirikiana na upande wa Mashtaka kutoa ushahidi wa uongo.
Aidha, Kenyatta anasema kuwa mashahidi wake wametishwa na upande wa Mashtaka na kulazimishwa kubadilisha ushahidi wao.
Ombi hili la rais Kenyatta linakuja siku mbili tu baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Amina Mohammed kusema kuwa hakuna rais yeyote duniani ambaye amewahi kushtakiwa katika Mahakama hiyo au Mahakama nchini mwake akiwa uongozini.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu nchini Kenya mapema mwaka huu rais Kenyatta aliahidi kushirikiana na Mahakama hiyo hata kama angechaguliwa kuwa rais na kusema kuwa kesi inayomkabili ilikuwa ya kibinafsi.
Kikao cha Umoja wa Afrika kisichokuwa cha kawaida kitafanyika siku ya jumamosi jijini Addis Ababa Ethiopia kujadili uhusiano kati ya mataifa ya Afrika na Mahakama hiyo ya ICC.
Bunge la Kenya mwezi uliopita lilipitisha mswada wa Kenya kujiondoa katika mkataba wa Roma unaotambua Mahakama hiyo na kutoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano huo.
Hata hivyo, juma hili serikali ya Nairobi ilikanusha madai ya kutaka kutumia kikao hicho cha Umoja wa Afrika kuyashawishi mataifa mengine ya Afrika kujiondoa katika mkataba huo.
Awali Umoja wa Afrika uliomba kesi inayowakabili viongozi wa Kenya kurudishwa nyumbani kwa madai kuwa kuwepo kwao Hague kungehitilafiana na uongozi wao kama viongozi wa Kenya.
Naibu rais William Ruto ambaye kesi yake inaendelea katika Mahakama hiyo anarejea nchini Kenya Ijumaa usiku ili kumruhusu rais Kenyatta kuhudhuria kikao hicho cha Umoja wa Afrika .
Katiba ya Kenya hairuhusu rais na naibu wake kuwa nje ya nchi hiyo kwa wakati mmoja.
Ruto anatarajiwa kurejea mjini Hague siku ya Jumapili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi