Rais Obama na viongozi wa Republican |
Rais wa Marekani Barack Obama amekutana na wabunge wa
Republican kujadili kupitishwa kwa Bajeti ili kufungua huduma za
serikali ambazo zilikwama wiki iliyopita kwa ukosefu wa fedha.
Obama na wabunge wa Republican wamesema kuwa kikao hicho cha
dakika 90 kilikwenda vizuri lakini hadi sasa hakuna uamuzi wowote
uliochukuliwa.
Wabunge wa Republican wamempendekezea rais Obama kuendelea kuzungumza nao ili kupata suluhu la kudumu baada ya pande zote mbili kushindwa kuafikiana kuhusu kupitishwa kwa Bajeti hiyo.
Ikiwa suluhu halipatikana kufikia tarehe 17 mwezi huu Serikali ya Marekani itakosa fedha kwa kufikia kiwango chao cha mwisho cha kukopa fedha za kuendesha shughuli za serikali.
Awali, Spika wa bunge la Congress na kiongozi wa Wabunge wa Republican John Boehner aliwaambia waandishi wa Habari kuwa wao wako tayari kumsaidia rais Obama ili huduma za serikali zirejelewe na kumtuhumu kwa kukataa mazungumzo.
Rais Obama mapema juma hili aliwaambia wanasiasa wa Republican kuwa ni kama watu ambao wanataka kikombozi ili kufanya kazi yao.
Maelfu ya wafanyikazi wa Serikali nchini humo wako nyumbani baada ya kukosa kazi kwa kutokuwepo kwa fedha za kufanikisha huduma muhimu za serikali baada ya wabunge wa Republican kukataa kupitisha bajeti hiyo muhimu.
Shirika la fedha duniani IMF linasema kuwa ikiwa suluhu halitapatikana huenda likaathiri pakubwa uchumi wa Marekani na dunia nzima kwa kubwa.
Wabunge wa Republican wanasema kuwa walichukua hatua hiyo, ili kuchelewesha sera ya raia Obama kuhusu bima ya afya, mpango ambao rais Obama ameendelea kusisitiza kuwa hautabadilishwa.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!