Rais wa Malawi Joyce Banda amewafuta kazi Mawaziri wake 25 kwa tuhuma za ulaji rushwa katika serikali yake.
Rais wa Malawi Joyce Banda |
Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakimtaka rais Banda kukabiliana na ufisadi katika serikali yake ili kuendelea kupata ufadhili wa kifedha kwa kuhakikisha kuwa inawaadhibu wanaopatikana na kosa.
Umoja wa Ulaya unatarajiwa kutoa ufadhili wa Euro Milioni 29 mwezi Desemba mwaka huu kuimarisha Bajeti yake kuendelea ufadhili wa asilimia 40 kutoka kwa mataifa ya Magharibi.
Ripoti zinasema kuwa kuna baadhi ya maafisa wa serikali waliopatikana na kiasi kikubwa cha fedha nyumbani kwao wakiwa wamezificha mvunguni kwa kitanda.
Inashukiwa kuwa kifo cha Mphwiyo ambaye alikuwa ni Mkurengenzi wa Bajeti ya serikali kunaonesha kuwa alikuwa mlengwa na maafisa wengine wa serikali ambao walihofia wangekamatwa.
Wiki iliyopita, maofisa tisa wa serikali walitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka na baadaye kufungwa jela miaka 14.
Rais Banda amesema kuwa ataliteua Baraza lingine la Mawaziri katika siku chache zijazo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!