Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Written By Unknown on Thursday, 17 October 2013 | Thursday, October 17, 2013




Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.

Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.

Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss:Bakariiii!
Bakari:Naam baba!
Boss:nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss:Bakariiiii !
Bakari:naam baba!
Boss:nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.

Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari:baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.

Bakari:Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari:Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss kimyaaaa!
Bakari:Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari:Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss kimyaaaaaaa!

Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi