Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Shirika la kupambana na silaha za Kemikali latapa tuzo la Nobel

Shirika la kupambana na silaha za Kemikali latapa tuzo la Nobel

Written By Unknown on Friday, 11 October 2013 | Friday, October 11, 2013

.
Shirika la Kimataifa la kuzuia matumizi ya silaha za kemikali duniani OPCW, limetangazwa mshindi wa tuzo la amani la Nobel mwaka 2013.

Kamati ya kutoa tuzo hiyo imetangaza mshindi siku ya Ijumaa mjini Oslo nchini Norway kuwa shirika hilo lililobuniwa mwaka 1997 kupambana na matumizi ya silaha za Kemikali ili kuimarisha usalama duniani.
Hii inaamisha kuwa Shirika hilo sasa litapata Dola Milioni 1 nukta 25 kama tuzo katika juhuzi zake za kuhakikisha kuwa silaha hizo hazitumiwi na dunia inakuwa sehemu salama ya kuishi.
Tuzo hilo limetolewa wakati shirika hilo likiwa nchini Syria kuteketeza silaha za kemikali zinazomilikiwa na serikali ya rais Bashar Al Assad ambaye anatuhumiwa aliruhusu jeshi lake kuzitumia mwezi Agosti mwaka huu kuwashambulia wapinzani na kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Mwanafunzi kutoka nchini Pakistan Malala Yousafzai aliyepigwa risasi na kundi la wanamgambo wa Taliban na kutibiwa nchini Uingereza, Daktari Denis Mukwege anayetoa matibabu kwa wanawake wanaobakwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni miongoni mwa watu waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hilo.
Wengine waliokuwa katika orodha hiyo ni pamoja na Chelsea Manning ambaye pia anafahamika kama Bradley Mannning aliyetoa siri za serikali ya Marekani na Maggie Gobran, Mwanasayansi kutoka nchini Misri aliyeachana na kazi yake na kuanza kuwahifadhi watoto katika Kanisa la Coptic.
Tuzo la Nobel hutolewa kila mwaka kumtuza mtu aliyesaidia kuleta amani au mabadiliko muhimu kwa jamii na ilianziswa na raia wa Sweden Alfred Nobel mwaka 1895.
Mwaka 2012 Umoja wa Ulaya ulipewa tuzo hilo la amani katika juhudi zake za kuleta mabadiliko ya kiuchumi, siasa na amani barani Ulaya.
Miongoni mwa viongozi ambao wamewahi kushinda tuzu hilo ni pamoja na rais wa Marekani Barrack Obama mwaka 2009, na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi