Samantha
Lewthwaite aka The White widow au Mjane mweupe anatafutwa na polisi na
vyombo vya usalama karibu dunia nzima akiwa mshukiwa namba moja wa tukio
la ugaidi lililotokea huko Westgate nchini Kenya siku kadhaa
zilizopita.
Imefahamika kuwa mwanamke huyu ambaye ni mama wa watoto wanne, kwa muda fulani alikuwa ameolewa kwenye ndoa halali na mume ambaye ni raia wa kenya ambaye ni mwanajeshi kwenye kikosi cha jeshi la maji.
Mume wake ambaye ametajwa ni Abdi Wahid magazeti yameripoti kuwa yuko Ulaya na ushahidi mwingine unaonyesha kuwa mwanamke huyu ambae ni mama wa watoto wanne akiwa amebadilisha dini toka Ukristo na kuwa Muislamu alishiriki kwenye tukio la ugaidi wa Westgate na baadae akafanikiwa kutoroka.
Taarifa hizi hata hivyo zimekanushwa na mamlaka nchini Kenya ambazo zinadai kuwa hazina taarifa yoyote juu ya mwanamke huyo gaidi kuolewa na Mkenya, mume wa zamani wa Samantha ni Jermaine Lindsey alikuwa gaidi kama samantha na alijilipua na kufariki wakati akijaribu kufanya tukio la ugaidi huko London mwaka 2005.
Samantha alikuja Afrika mwaka 2009 na kwa kipindi cha miaka miwili amekua akikimbiakimbia huku na kule..
. |

Wahid alikamatwa mwaka 2011 baada ya polisi kugundua kwamba nyumba
yake huko Mombasa iligeuzwa kuwa kiwanda cha kutengeneza mabomu na mkewe
ambae ni Lewthwaite ambapo Wahid hakuwahi kuhukumiwa na alitambulika
kama mwenye nyumba kwa mujibu wa ripoti za magazeti na haikuwekwa wazi
alikua anaujua Ugaidi wa mke wake kiasi gani.
Saa kadhaa zilizopita kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab kimesisitiza
kwamba hakuna Mwanamke yeyote aliejiunga nao kwenye kufanya mashambulio
ya Nairobi kwenye mall ya Westgate hivyo hiyo imemaliza utata kwamba
Mwanamke huyo alitumwa na Al Shabaab kwenye mashambulio hayo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!