Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UHUSIANO WA WASANII NORA NA GEOFREY KUSILA WAVUNJIKA....

UHUSIANO WA WASANII NORA NA GEOFREY KUSILA WAVUNJIKA....

Written By Unknown on Friday, 11 October 2013 | Friday, October 11, 2013


UHUSIANO wa wasanii wawili wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Geofrey Kusila umeota mbawa baada ya kumwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.

Chanzo kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.

“Nora na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake hata kazi hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa kipindi chake kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:

“Mimi ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa sababu tumeachana na kampuni ambayo tulikuwa tumeianzisha nayo imekufa na baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake na kuangalia jinsi gani atakavyofanya kazi hivyo hatupo pamoja tena.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi