Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » UJUMBE TOFAUTI WAINGIA BAIDOA NA HUKU IKIJIANDAA KWA MKUTANO WA MKOA

UJUMBE TOFAUTI WAINGIA BAIDOA NA HUKU IKIJIANDAA KWA MKUTANO WA MKOA

Written By Unknown on Saturday, 19 October 2013 | Saturday, October 19, 2013


Mamia ya vikosi vya usalama vya ndani vinafanya doria ya saa 24 kuimarisha usalama huko Baidoa kabla ya mkutano wa kuundwa kwa serikali ya shirikisho kwa mikoa sita ya Somalia ya kusini.
Mikoa iliyojumuishwa katika mkutano, uliopangwa kuanza tarehe 20 Oktoba, ni pamoja na Bay, Bakol, Gedo, Jubba ya Kati, Jubba ya Chini na Shabelle ya Chini.
Bado mikoa mitatu kati ya mikoa hii -- Gedo, Jubba ya Kati na Jubba ya Chini -- ambayo tayari ziliungana kuunda utawala wa muda wa Jubba (IJA), iliyothibitishwa na makubaliano yaliyofikiwa mwishoni mwa mwezi Agosti kati ya serikali ya shirikisho ya Somalia na viongozi wa utawala wa kimkoa wa Jubbaland huko Addis Ababa, Ethiopia.
"Kuunda utawala kwa majimbo sita ni kinyume na makubaliano ya Addis Ababa," alisema Abdirahman Omar Yarisow, msemaji wa serikali ya Somalia.
Serikali ya shirikisho haitahusika katika mkutano wa Baidoa, aliiambia Sabahi, akiongezea kwamba serikali itaunga mkono makubaliano ambayo yatakuwa yameafikiwa miongoni mwa umma, lakini siyo kuunda tena utawala mpya kwa mikoa ya Jubba na Gedo.
Yarisow alitoa wito kwa wawakilishi wa Jubba na Gedo wanaopanga kukutana huko Baidoa badala ya kujengwa juu ya utawala ambao tayari ulishanzishwa kwa mikoa yao, ikiongozwa na kiongozi wa muda Sheikh Ahmed Mohamed Islam Madobe, na kuwa sehemu katika mazungumzo ya usuluhishi yanayolenga kusuluhisha masuala yaliyobakia.
Baadhi ya makabila ya mikoa ya Jubba na Gedo yalielezea kwa uwazi kwamba waliachwa nje ya mchakato unaongozwa na Kismayu kuunda serikali ya shirikisho ya Jubbaland ambayo ilitokana na uchaguzi wa Madobe, na kwa hiyo haiungi mkono IJA.

Ujumbe mchanganyiko

Watawala huko Baidoa na katika mikoa mingine walihusishwa, hata hivyo wanadai kwamba wanaungwa mkono na serikali ya shirikisho -- kwa jina, Spika wa Bunge Mohamed Osman Jawari -- na wataendelea na mkutano huo kama ulivyopangwa.
Naibu gavana wa mkoa wa Bay Shina Moalim Nur alisema jitihada zimesaidia uwakilishi wa mikoa sita iliyohusishwa, na kwamba makubaliano ya serikali ya shirikisho yaliyofikiwa na Madobe hayakuwa na msingi.
"Rais, waziri mkuu na mawaziri waliosaini makubaliano ya Addis Ababa, hakuna mmoja wao aliombwa ushauri kuhusu mkutano wa Baidoa wa kuunda utawala wa majimbo sita, lakini Spika wa Bunge Jawari anajua kuhusu mkutano na anauunga mkono," aliiambia Sabahi. "Spika wa bunge pamoja na wabunge 50 wanaowakilisha mkoa walizindua mazungumazo [ya awali] na hatuhitaji ridhaa kutoka kwa yeyote yule."
Nur alisema serikali ya shirikisho ilikutana naye na kumuagiza kusimamisha mkutano, lakini alisema alikataa kwa sababu anaaminiwa na watu wake.
Jawari hakujibu maswali mengi ya Sabahi kwa ajili ya maoni, lakini ikiwa madai ya Nur ni kweli, inaweza kuashiria kutoungana kati ya serikali na uongozi wa bunge katika mchakato wa kuunda utawala wa shirikisho wa mkoa.

Kuwasili kwa wajumbe

Hata hivyo, zaidi ya wajumbe 650 kutoka Somalia nzima na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa Baidoa, kwa mujibu wa Kaimu Kamishna wa Muda wa Baidoa Abdulkadir Sheikh Ali.
Kuandaa mazingira tofauti ya usalama yaliyoanzishwa kutokana na kuingia kwa wingi kwa ujumbe, Baidoa imesambaza vikosi 400 vya usalama vya ndani na kuweka vituo 14 vya upekuzi katika jiji zima na vituo vya kuingilia ili kukagua magari ya abiria, aliiambia Sabahi.
Ali alisema alifurahi kwamba Baidoa ilichaguliwa kuandaa mkutano huo. "Tumekuwa hatuaminiki kwa kazi hii na serikali ya Somalia pamoja na msaada kutoka kwa umma na wazee wa mila kutoka katika mikoa hii sita," alisema.
Ali alisema Baidoa imelindwa na kuvishukuru vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) vilivyopo jijini kwa msaada wao unaoendelea katika kuhakikisha usalama wa wakaazi wa Baidoa.
Kwa upande wake, Kapteni Annatole Ciza, msemaji wa kikosi cha Burundi huko Baidoa, alikariri wajibu wa AMISOM wa kuhakikisha usalama na kuhimiza mazungumzo huko Somalia.
"Tunawahamasisha Wasomali kuchagua amani na kuepuka kitu chochote ambacho kitazuia usalama," alisema, akiongeza kwamba vikosi hivyo vitaendelea kutofungamana na upande wowote.
Kama haukuzuiliwa, mkutano utaendelea kwa mwezi mmoja na fedha zitatolewa na wakaazi wa ughaibuni kutoka katika mikoa sita, pamoja na wafanyabiashara wenyeji, alisema Ali.
"Sasa tuna kazi nyingi kuwakaribisha wageni katika mkutano, baadhi yao wanatoka nchi za nje," alisema Abdullahi Adam Ali Shaleyte, mjumbe wa kamati ya mkutano na mbunge wa zamani katika Serikali ya Shirikisho ya Mpito.
"Hali ya usalama, ambayo imefanya uwezekano kwetu kuamua kuitisha mkutano huko Baidoa, ni moja ya mambo ambayo tunajivunia sana," aliiambia Sabahi. "Tuna matumaini ya juu kwamba mkutano huu utakuwa na matokeo mazuri ya maendeleo katika miezi iliyopangwa na sasa hatufikirii kama muda zaidi utahitajika"
Dahir Bakar, mzee mwenye umri wa maiaka 54 kutoka Mkoa wa Shebelle ya Chini, anahudhuria mkutano huo na alielezea matumaini yake kwamba utafanikiwa katika kuanzisha utawala wa pamoja wa mkoa kwa watu wa mikoa hiyio sita.
"Nina matumaini kwamba hakutakuwa na migogoro ambayo itasababisha ucheleweshaji wa muda mrefu wa kutafuta utatuzi wa kisiasa [kwa masuala yanayoendelea], kama tulivyotarajia kwa utawala mwingine wa mkoa," alisema. "Kama wajumbe wa mkutano, tunajitahidi kuweka matakwa ya umma wa Wasomali kabla ya matakwa ya mtu mwingine yeyote."
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi